Siasa za bongoland: Ukiwa upande wowote (CCM au UPINZANI) lazima uwe tayari kutetea UDHAIFU

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Kinachotokea katika siasa za bongoland hadi sasa, wanasiasa wote wa Upinzani na watawala wanamapungufu na faida katika mienendo yao.

Kwa harakaharaka, Udhaifu mkubwa hauonekani kwa viongozi wa kisiasa bali wafuasi wa vyama au viongozi hawa. Wafuasi hasa huku mitandaoni watatumia kila mbinu Matusi, Hoja nzito,Mashairi,Picha, Video clips, Mafungu ya vitabu vitakatifu, Quotes za watu maarufu wa zamani ili kumtetea mwanasiasa wampendae katika hali yote. Yaani Kama ni chadema atatetea chochote cha chadema kama ni perfect 100%, kama ni CCM atatetea vya CCM kama ni perfect 100% kwa gharama yoyote ile na kama mko karibu hata ngumi utakula. Mwenendo huu umepelekea kuwapa nafuu wanasiasa na kuwadumaza katika udhaifu wao.


Kuna sababu nyingi, kwa nini Bongoland ni masikini.

NB: Mimi sina chama cha siasa ila navutiwa zaidi na itikadi ya CCM katika misingi yake ile wakati inaanzishwa ambayo kama ingefuatwa tunavyolalamikia visingekuwepo.
 
Siasa inafanywa na binadamu na kama ujuavyo sio wakamilifu na tunawaza tofauti.Tatizo ni pale mmoja au kundi fulani kujifanya ni malaika au miungu watu wasiokubali kukosolewa.We're all still learning at some point
 
Back
Top Bottom