Siasa za Bongo ni za Kikatuni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za Bongo ni za Kikatuni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Mar 31, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siasa za nchi hii huwa hazieleweki kabisa. Ni siasa zilizojengwa katika misingi ya kuburudishana na kufurahishana. Kama mtu ni CCM hata kama chama chake kinakosea basi atakitetea mpaka mijasho inamtoka, na akiwa wa chama kingine hata kama chama hicho kinapotea yeye "atakomaa" hata kwa kutoa mitusi ya nguoni.

  Siasa zetu hakuna hoja inayobishaniwa. Kenya kwenye uchaguzi wao ujao hoja ni nani anaweza kuijenga Kenya isiyo na ukabila, Marekani hoja ni kama Bima ya Afya iliyopendekezwa na utawala wa Obama inafaa au haifai. Hapa kwetu hoja ni kama Vincent ni mtoto wa Nyerere au siyo!!

  HIZI NI SIASA ZA KIKATUNI!!
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hicho kilikuwa kijembe. hoja arumeru ni ardhi na maji.
   
 3. B

  Baruni Senior Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu umenena.
   
 4. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo hili ni la kwetu sote sisi watanzania. Ardhi na maji ni matatizo ya Arumeru lakini ni nani aliyejenga hoja jadidi kuhusu matatizo ya Maji na Ardhi Arumeru? Tutofautishe kati ya ahadi na uchambuzi yakinifu. Kwa mfano Ardhi kwa mazingira ya sasa huko Arumeru haiwezi kugawiwa bure, ni lazima mashamba ya watu binafsi au ya serikali ndiyo yatolewe ili watu wa Arumeru wapate Ardhi ya kutosha.

  Ni nani aliweza kutuambia watu wa Arumeru wako wangapi, wasio na Ardhi ni wangapi, kati ya hao wasio na Ardhi ni Asilimia ngapi wanaishi chini ya Dola moja kwa siku hivyo watashindwa kununua Ardhi hiyo hata kama itauzwa leo hii, na ni nini kitafanywa ili watu hao nao wamiliki Ardhi?

  Hivi Ardhi inayotakiwa ni kwa ajli ya Kilimo au Makazi. Kama ni kwa Kilimo ni Kilimo cha aina gani, cha umwagiliaji au cha kusubiri mvua inayokuja kwa kudra za Mwenyezi mungu. Jee kule kwenye Ardhi tele na mvua za kutosha kilimo kimefanikiwa au ni mbinu zipi zitatumika kufanikisha kilimo hicho Arumeru?

  Jee tatizo la Ardhi kwa watu wa Arumeru haliwezi kutatuliwa nje ya Arumeru kama lilivyotatuliwa tatizo la Ardhi Moshi Miaka ya themanini. Tija inayopatikana kutokana na matumizi ya Ardhi Arumeru inalingana na nguvu inayowekezwa na wanaomiliki Ardhi Arumeru? Jee wamiliki wa mashamba makubwa wanyang'anywe Ardhi wanayoimiliki bila kuitumia au wahimizwe kuitumia kama sharti la kuendelea kuimiliki Ardhi?

  Kuhusu maji nimesikia ahadi toka kwa vyama vyote (siyo toka kwa wagombea) vyenye wagombea Arumeru, lakini zote ni "ahadi" tu. Sijasikia kama kuna mtu anatoa ahadi zake kwa kuegemea utafiti wa kisayansi kwamba maji yaliyopo Arumeru yanatosha au hayatoshi kugawiwa kwa wana Arumeru wote. Ni shilingi ngapi zitahitajika kwa ajili ya kuwekeza kwenye mradi wa kupeleka maji kwa sehemu kubwa ya wana Arumeru.

  Pia sijasikia kama kuna mtu ameelezea kinaga ubaga kwamba Arumeru kuna vyanzo vingapi vya uhakika na endelevu vya maji. Au kuna mkakati gani unaotarajiwa kufanywa ili kutunza vyanzo hivyo vya maji na maji yanayopatikana sasa yanatolewa kwa kiwango cha chini kwa asilimia ngapi na ili kuiongeza hiyo asilimia kifanyike nini?

  Siamini kama hakuna mabishano ya hoja, KIJEMBE huwa kinaleta ladha yoyote kwenye mazungumzo!! Suala la uzao wa Vincent Nyerere lisingekuwa kubwa kiasi kile kama kilikuwa ni KIJEMBE tu!! Hivi ndivyo tunavyoendesha siasa zetu KIKATUNI!!

   
 5. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila mtu ana maono yake katika maisha. Mimi naamini sana katika mapinduzi ya umma kama ilivyofanyika Tunisia na Misri, sikuunga mkono kilichotokea Libya. Lakini hiki cha Mali nimekipenda sana.

  Nimeandika katika thread yangu "KWA HILI, 2015 NI MBALI SANA". Yako mengi, lakini kubwa ni kwamba, mimi namuona CCM kama adui wa nne, lakini wakati huo huo wa kwanza kwa watz ukiongeza wale watatu ambao Mwl. Nyerere aliwatangaza baada ya uhuru ambao hivi sasa wameongezeka kwa kasi. Bila kuunganisha nguvu, tukaweka tofauti za dini zetu, kabila zetu na itikadi za kisiasa kando, HAKIKA NAWAAMBIA, kuiondoa CCM mdarakani, ni kazi sana. Hadi siku ambayo askari polisi watakapojitambua, wanajeshi wakajitambua ndipo tutaona ukombozi halisi wa TAIFA HILI. Kama askari polisi wanaridhikia na elfu 50000/- ambazo wanalipwa kuwapiga wananchi mabomu, bado taifa liko chini ya UKOLONI WA CCM na kibaraka wake MMAREKANI.
   
 6. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni lazima tuhakikishe UKOMBOZI wa Kweli unakuja kwa kuleta mabadiliko ya fikra na si mabadiliko ya washika madaraka.
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kwamba mabadiliko ya fikra kwa wananchi ni muhimu kama tunataka kuwaondoa hawa madhalimu madarakani kwani wanawahonga washika bunduki kama ndio bima yao ya kuendelea kututawala!
   
 8. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Walivyo mazezeta hawatajifunza lolote kutoka kwenye uchaguzi huu. Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa.
   
Loading...