SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA

Bukinabuza

Senior Member
Jun 17, 2008
105
29
Nawauliza wana JF hii siasa ya ujamaa na kujitegemea bado iko kwenye katiba yetu? au CCM waliitupilia mbali bila wananchi kuelezwa. Nimeambiwa kuwa Magufuli ana mpango wa kutaifisha ma bank yote

Hii imekaa je?
 
Nawauliza wana JF hii siasa ya ujamaa na kujitegemea bado iko kwenye katiba yetu? au CCM waliitupilia mbali bila wananchi kuelezwa. Nimeambiwa kuwa Magufuli ana mpango wa kutaifisha ma bank yote

Hii imekaa je?
Kama siasa hiyo imefutwa au bado sijui lakini haipo tena na sidhani kama mheshimiwa rais anafikiria kutaifisha chochote sababu itakuwa ni kujiweka kitanzi cha uchumi kuanguka na kuanza foleni za kila kitu badala ya uzalishaji !! sababu wengi wanaokabidhiwa wanataka kula.
 
Siasa ya ujamaa na kujitegemea ya Nyerere aliifutilia mbali Raisi Mwinyi wakati mwenyewe Nyerere yuko hai, ni siasa za kijinga zilotucheleweshea maendeleo! hii nchi ni kama ilipata uhuru mwaka 1985 baada ya Mwinyi kulifuta hili li siasa ya ujamaa na kuifungua nchi ilokuwa ya giza, atleast miji ikaanza kupanuka na watu kuona duniani kuna nini, sio kila siku kushinda kwenye foleni la sukari na mafuta kwenye maduka ya kaya!
 
Atataifishaje mabank mkuu,usidhani kila kitu rais anaweza kufanya,yes a President has got prerogative powers lakini sio kwenye kila kitu,currently sisi kama nchi we are in mixed economies,so huwezi kutaifisha mabank kama ulivyoota hapo juu,ili nchi iendelee popote duniani huwezi kuacha masuala nyeti kama hayo ya Uwekezaji,vinginevyo nchi itateteleka kimapato n.k.....,haya mabank hayakuchipua tu toka ardhini,kuna sheria,kanuni na taratibu mbalimbali zinafuatwa ili kuwepo,sidhani rais sio mtu wa kufuata sheria akafanya hayo uyasemayo,zaidi ya yote naomba niamini haukua serious kwenye andiko lako!
 
Back
Top Bottom