xpin de rexas
Member
- Feb 3, 2013
- 26
- 2
Mimi nashangaa vijana tunabishana kuhusiana na vyama vya siasa....tena mpaka kutukanana.Mimi kama mimi siangalii CCM,CHADEMA wala CUF ila maendeleo kwa vijana na watanzania kwa ujumla.Siasa itabaki kua siasa ndivyo ilivyo mwenye kiti anampaka mavi mpinzani ili andelee kukalia kiti na mpinzani anampaka mavi mweyekiti kumng'oa kwenye kiti.Siasa ya Tanzania bado haijakomaa si chama tawala wala vyama pinzani.Maendeleo yanaletwa na mpango mkakati wa Taasisi imara yenye watu imara ndani yake si kwamba CHADEMA au chama chochote pinzani kikiingia kesho madarakani kwamba kila mtanzania baada ya miaka mitano ataishi maisha bora.Tuangalie kwanza nchi imetoka wapi....kuna ukoloni mambo leo,mikataba toka enzi ya wakoloni hvi ni vitu vyote ambavyo vinazidi kuitokomeza Tanzania yetu.Tunataka Rais ambaye atakua na ushupavu wa kuitoa nchi katika dimbwi hili.Haito jalisha anatoka chama gani.Vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa hili.Uchama wetu hauto tufikisha popote.Maana sasa hvi nchi inaenda kubaya kutokana na siasa mbovu ya vyama vyote.na sisi vijana tuko mstari wa mbele kila mtu akisimamia upande wake wa chama chake...hakuna tutakacho vuna.Tupime yanayo fanyika wakati huu.2015 wasomi hasa vijana tunakazi ya kumpima Rais wa nchi yetu na kuangalia uwezo wake wa kuiongoza nchi yetu na kuitoa kwenye dimbwi la umaskini pasipo kuangalia chama cha siasa kwasababu huwezi kuwekewa mtu asiye na mpangilio eti kwa sababu ni mgombea wa CCM,CHADEMA,CUF au chama chengine chochote na kuipima ilani ya chama chake pasipo kukurupuKa kwani ndiyo tuanvyo fanya kwa kufuata mkia au upepo.
MAENDELO YA TANZANIA YANALETWA NA SISI WANANCHI KWA KUCHAGUA JEMBE LENYE MAKALI NA SIO BORA LIENDE.
#kama haukubaliani na mimi haitosaidia pia....
MAENDELO YA TANZANIA YANALETWA NA SISI WANANCHI KWA KUCHAGUA JEMBE LENYE MAKALI NA SIO BORA LIENDE.
#kama haukubaliani na mimi haitosaidia pia....