Bwege2030
Member
- May 10, 2025
- 82
- 152
MISINGI YA KUJENGA UTAJIRI
~Watu wengi huchanganya Mshahara mkubwa na Utajiri,Lakini utajiri wa kweli ni mfumo unaojitegemea.
Badala ya kuwa mpangaji tu au dereva wa taxi,lengo liwe kumiliki fremu za maduka, mashamba ya mazao ya biashara kama mibuni au michikichi au hisa kwenye makampuni makubwa kama TBL, NMB, au Vodacom kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
sababu hukua thamani hata ukiwa umelala.
Utajiri wa kweli ni uwezo wa kuamua nini cha kufanya na muda wako.
Ikiwa kipato chako kinategemea uwepo wako wa saa 24, wewe ni Mshughulika lakini bado hujawa Tajiri.
Tajiri ni yule anayeweza kwenda kijijini kwao kwa mwezi mmoja kuhani msiba au kupumzika na bado biashara yake ya Kariakoo au duka lake la jumla likaendelea kumpatia faida bila yeye kuwepo.
Badala ya kusimamia mwenyewe kila mteja anayekuja kwenye gereji yako weka mfumo wa risiti, meneja na fundi mkuu. Mfumo unahakikisha kazi inafanyika kwa ubora uleule hata kama wewe haupo.
Wengi huingia kwenye miradi ya UPATU au Cryptocurrency zisizoeleweka wakitaka utajiri wa haraka na kuishia kupoteza kila kitu.
Uvumilivu ni kama kupanda miche ya mitiki inachukua miaka lakini ikikomaa, unakuwa na utajiri wa uhakika.
Ukianzisha huduma ya kusafisha ofisi au kupeleka chakula maofisini kwa usafi na muda sahihi, unatatua kero ya wafanyakazi wengi. Thamani hiyo ndiyo itakayokuletea pesa.
Usiulize "Nipate wapi hela?", uliza "Nitatue tatizo gani la watu?"
Ni kusema hapana kwa kununua gari la kifahari la mkopo wakati bado hujawekeza kwenye kiwanja au biashara inayojitegemea. Nidhamu ni kuzuia kuvuja kwa fedha kwenye sherehe zisizo na tija na kuelekeza fedha hiyo kwenye uwekezaji.
Pesa ni kama maji kwenye ndoo yenye matundu.Bila Nidhamu, ndoo itabaki tupu. Bila Mifumo, utachoka kuchota maji. Bila Umiliki, unachota maji kwa ajili ya ndoo ya mtu mwingine.

Utajiri hauji kwa kufanya kazi pekee,unakuja kwa kumiliki kile kinachozalisha thamani.Ukifanya kazi ya kuajiriwa tu, kipato chako kina kikomo.
Badala ya kuwa mpangaji tu au dereva wa taxi,lengo liwe kumiliki fremu za maduka, mashamba ya mazao ya biashara kama mibuni au michikichi au hisa kwenye makampuni makubwa kama TBL, NMB, au Vodacom kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
sababu hukua thamani hata ukiwa umelala.
Utajiri wa kweli ni uwezo wa kuamua nini cha kufanya na muda wako.
Ikiwa kipato chako kinategemea uwepo wako wa saa 24, wewe ni Mshughulika lakini bado hujawa Tajiri.
Tajiri ni yule anayeweza kwenda kijijini kwao kwa mwezi mmoja kuhani msiba au kupumzika na bado biashara yake ya Kariakoo au duka lake la jumla likaendelea kumpatia faida bila yeye kuwepo.
Jitihada za kubahatisha huleta matokeo ya kubahatisha.Mifumo huondoa kubahatisha.
Badala ya kusimamia mwenyewe kila mteja anayekuja kwenye gereji yako weka mfumo wa risiti, meneja na fundi mkuu. Mfumo unahakikisha kazi inafanyika kwa ubora uleule hata kama wewe haupo.
Compounding inahitaji muda.Utajiri ni mbio za maratoni, sio mbio fupi za mita 100.
Wengi huingia kwenye miradi ya UPATU au Cryptocurrency zisizoeleweka wakitaka utajiri wa haraka na kuishia kupoteza kila kitu.
Uvumilivu ni kama kupanda miche ya mitiki inachukua miaka lakini ikikomaa, unakuwa na utajiri wa uhakika.
Fedha ni matokeo ya kutatua matatizo ya watu wengine.Soko halilipi jitihada soko hulipa suluhisho.
Ukianzisha huduma ya kusafisha ofisi au kupeleka chakula maofisini kwa usafi na muda sahihi, unatatua kero ya wafanyakazi wengi. Thamani hiyo ndiyo itakayokuletea pesa.
Usiulize "Nipate wapi hela?", uliza "Nitatue tatizo gani la watu?"
Ni kupambana na Lifestyle Inflation kuongeza matumizi kila mshahara unapoongezeka.Nidhamu ni kusema Hapana kwa mambo ya anasa ili kulinda mtaji.