Siasa ya kweli duniani ni ile ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo Tanzania ilitushinda kitambo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,966
141,974
Itikadi ya ujamaa na kujitegemea ndio siasa pekee yenye usawa na kutenda haki hapa duniani lakini kwa kuwa ulimwengu huu umeelemewa na siasa za UONGO na uzushi siasa za ujamaa zimefutika kabisa.
Ujamaa ni Imani na wale wote wanaoamini katika ujamaa nyuso na matendo yao huonyesha hilo na si huu ujamaa wa maneno tunaousikia.

Katika hili niwapongeze sana CHADEMA kwa kuwa wakweli kuhusu itikadi inayowaongoza yaani ubepari pamoja na kwamba practice yao imekaa kiuchwara uchwara lakini kwa mbali wanajsribu kufanana nayo.

Kule CCM ni kama alivyosema rip Komba kwamba "CCM ni kokoro" lililosheheni visafi na vichafu hivyo si rahisi hata kuelewa itikadi yake ndio maana watu kama Madabida wanafukuzwa na kurejeshwa kirahisi mno.

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
 
Unajua Kuwa 1992 CCM iliachana Na Siasa ya Ujamaa Na kujitegemea kwa ku replace Azimio la Arusha kwa Azimio la Zanzibar?

Wewe Ni Mwana CCM gani huheshimu Vikao halali vya Chama vilivyofuta Azimio lile?
 
Katika hili niwapongeze sana Chadema kwa kuwa wakweli kuhusu itikadi inayowaongoza yaani ubepari pamoja na kwamba practice yao imekaa kiuchwara uchwara lakini kwa mbali wanajsribu kufanana nayo.

Kule CCM ni kama alivyosema rip Komba kwamba "CCM ni kokoro" lililosheheni visafi na vichafu hivyo si rahisi hata kuelewa itikadi yake ndio maana watu kama Madabida wanafukuzwa na kurejeshwa kirahisi mno.

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
Umenena, ujamaa bado muda wake. Nilisomaga DS zamani kuwa ukitoka ubepari ndo unaenda ujamaa, kama Kule Scandinavian countries
 
Unajua Kuwa 1992 CCM iliachana Na Siasa ya Ujamaa Na kujitegemea kwa ku replace Azimio la Arusha kwa Azimio la Zanzibar?

Wewe Ni Mwana CCM gani huheshimu Vikao halali vya Chama vilivyofuta Azimio lile?
Kosa kubwa walifanya hawakubadili katiba, walimwogopa mwalimu nyerere, hata rasimu ya warioba haikuliweka sawa hili
 
Kosa kubwa walifanya hawakubadili katiba, walimwogopa mwalimu nyerere, hata rasimu ya warioba haikuliweka sawa hili

Wabadili Katiba ya nini?

1992 yalifanyika Marekebisho madogo ya Katiba kuruhusu Mfumo wa Vyama vingi lakin
Azimio la Arusha halikuwahi kuwemo Kwenye Katiba lilikuwa ndani ya Chama tu Na kuliondoa hapakuhitaji kubadili Katiba bali Azimio tu Kama lile la Zanzibar

Hivi karibuni TBC walimuhoji Mzee Mwinyi kuhusu Azimio la Znz na Umuhimu wake kwa wakati ule Na sasa lakin Cha kushangaza mjadala ule hau kurushwa kwa Kuwa ungewavua nguo baadhi ya Wajamaa Uchwara
Mf. Azimio lilipiga Marufuku Mtumishi wa umma Au Kiongozi Kuwa Na Nyumba ya kupangisha lakin sharti Hilo halikuwemo kwny Katiba ulikuwa sehemu ya Miiko ya Uongozi ndani ya TANU
 
We are two faceted!! Tunaupenda ujamaa ili tu tuonekane tuna 'utu' na Tuna practice ubepari kwa kuwa upo ndani ya human instinct! Hatuwezi kuuvua tu kama nguo! Demokrasia na ujamaa havikai pamoja! Demokrasia na ubepari ni kama kidole na kucha! Profesa kitila alinifundisha eti tunafuata mfumo wa siasa unaoitwa social democrat! Nikauliza je huo mfumo ni wa kijamaa? Au kibepari? Akasema ni 'demokrasia ya kijamaa' nikauliza tena je ni sahihi pia tukisema ni 'ujamaa wa kidemokrasia? Akasema of cause 'yes' but it lacks some standards to be "logical" hata sikumwelewa!!
 
Utasubiri sana kama unataka watu waporwe Mali zao walizozitafuta kwa jasho kwa siasa hovyo na fikra ambazo hazina uhalisia na za kipuuzi za ujamaa.

Kwa hakika kwa hili bara letu viongozi hao walioleta ujamaa baada ya Uhuru hapana shaka kabisa kuwa walileta ujamaa ili wawatawale vizuri waafrika sababu wangepata support ya masikini ambao ndio by far majority.

Huko USSR ambapo ndio ujamaa ulianzia na ulitekelezwa kuliko sehemu yeyote Viongozi wa serikali na chama cha kikomunisti waliishi maisha gani ukireflect na maisha ya watawaliwa?
 
Itikadi ya ujamaa na kujitegemea ndio siasa pekee yenye usawa na kutenda haki hapa duniani lakini kwa kuwa ulimwengu huu umeelemewa na siasa za UONGO na uzushi siasa za ujamaa zimefutika kabisa.
Ujamaa ni Imani na wale wote wanaoamini katika ujamaa nyuso na matendo yao huonyesha hilo na si huu ujamaa wa maneno tunaousikia.

Katika hili niwapongeze sana CHADEMA kwa kuwa wakweli kuhusu itikadi inayowaongoza yaani ubepari pamoja na kwamba practice yao imekaa kiuchwara uchwara lakini kwa mbali wanajsribu kufanana nayo.

Kule CCM ni kama alivyosema rip Komba kwamba "CCM ni kokoro" lililosheheni visafi na vichafu hivyo si rahisi hata kuelewa itikadi yake ndio maana watu kama Madabida wanafukuzwa na kurejeshwa kirahisi mno.

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
Ujamaa na kujitegemea si siasa ni mfumo unaokinzana hata unapoutamka.

Utakuwaje mjamaa hapo hapo unajitegemea? Fikiri.

Kitu kinachokinzana chenyewe kitatekelezeka vipi? Mzee yule naona siku aliyowazw hayo alikuwa katika hallucinations zake, kama kawaida ya uko wao.
 
Back
Top Bottom