VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Katika uchaguzi wa Urais nchini Marekani,nimejifunza kitu kimoja.Ni siasa safi. Kila mgombea-Obama na Romney alijikita kwenye sera zake na nini hasa utawala wake utafanya atakaposhinda. Hata Midahalo iliyoandaliwa ilijikita kwenye hoja za mustakabali wa Taifa. Ni mara mojamoja sana wagombea walipigana vijembe(lakini hasa kwa kukosoa mipango ya mwenzake na kuiona isiyotekelezeka).Siasa safi.Matokeo yalipotolewa,walipongezana na kutoa 'Hotuba za kushinda' na 'Hotuba za Kushindwa' Siasa safi
Hapa Tanzania,kwa umri wangu wa miaka 30 nimeshiriki kama mpiga kura chaguzi tatu: 2000,2005 na 2010. Wagombea wetu wengi hutukana,hukejeli,huchekesha,hujikweza,hudharau,huudhi na kukasirisha wagombea wenzao na wapiga kura.Kampeni nyingi hujaa matusi,kejeli,dharau na kadhalika. Wagombea hawajengi hoja. Siasa safi? Nchi itaendeleaje ikiwa mgombea ameingia madarakani kwa matusi,uongo,kejeli na dharau...bila hoja?! Siasa safi kweli hizi?
Siku nitakapogombea,nitaonesha mfano.Nikishindwa nikiwa safi, nitashukuru.Nikishinda, nitakuwa mfano wa kuigwa.Na hapo ndipo itakapoonekana kawaida kutokea siasa safi!