DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 409
- 343
Wanabodi,
Naomba tutazame kidogo nakala niliyo chapisha mara ya mwisho inayohusu mbinu kuu inayotumiwa na chama tawala (CCM) kubaki madarakani.
Lazima tukubaliane kwamba kama CCM ina ushawishi mkubwa kwenye sekta nyeti nchini, basi suala zima la kuwa na siasa za ushindani na ambazo wahusika hupingana kwa hoja ni ndoto ambayo bado hatuja itimiza. Sekta hizi nyeti ni kama
Kama mwananchi aliye guswa na mwenendo wa siasa nchini, ni vyema kama tunge kubaliana kwamba hali hii ni ngumu sana kubadilisha na hata kama uwezekano wa kurekebisha haya upo, itachukua muda mrefu sana. Swali la muhimu ambalo tunatakiwa kujiuliza ni kama vyama vyote vya siasa vinaweza kuendesha shughuli zao bila bugudha katika kipindi ambacho chama tawala kina ushawishi mkubwa na wafuasi wengi katika vyombo nyeti vya dola.
Fumba fumbua, lazima tuweze kuishi pamoja hata katika hali hii. kuishi vizuri pamoja kuna tegemea uwezo wa chama tawala kuwa "Responsible" katika suala zima la kuzuia vyombo hivi kuingilia uendeshaji na mambo ya ndani ya vyama vingine vya siasa.
Ni jambo nzuri kuona kwamba hatua zinachukuliwa kuhakikisha kwamba kuna maridhiano haswa kati ya CCM na CHADEMA lakini maridhiano haya yasi ishie tu kwenye runinga. Maridhiano ya kweli yanatakiwa kujumuisha mikakati ya kurekebisha utawala huu wa kidikteta, maridhiano ya kweli yanatakiwa yawafikirie wafungwa wote wa kisiasa. Makubaliano ya kweli ni yale yanayofanywa kwa kuzingatia itikadi na kwa kuamini kwamba siasa ni hoja. Kwasababu hiyo, hoja zako zinaweza kukubaliwa au kukataliwa na wananchi.
Mungu ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania

- Idara ya usalama wa taifa
- Jeshi la polisi
- Jeshi la wananchi (JWTZ)
- Mahakama n.k.