Siasa ndani ya vyama ziliwakataa Prof. Mwandosya na Salim A. Salim zikatuletea Jakaya Kikwete na hapa ndipo tulipo sasa

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
963
Reaction score
2,195
Tanzania na nchi nyingi za ulimwengu huu zinategemea vyama vya siasa kuzalisha viongozi wa kitaifa

Vyama vya siasa vina siasa ndani ya chama na vina siasa dhidi ya vyama vingine shindani hivyo kuna wakati kwao kipaumbele ni kuyapata madaraka pasipo kujali sana hulka, mitazamo, nguvu, wala uwezo wa huyo atakayeshika hayo madaraka

Kuna wakati kipimo chao huwa ni "nani anakubalika" zaidi kuliko wengine bila kujiuliza sana kwanini mtu huyo anakubalika na ametumia njia zipi hadi yeye kukubalika

Ndiomaa kesi za rushwa, hongo na kila aina ya ushawishi hutumika sana ndani ya vyama na hadi leo vimekosa mwarobaini kwasababu watu hutumia njia mbalimbali ili wakubalike

Jamii isiyo makini inayoendekeza siasa za vyama matokeo yake jamii hiyo itaendelea "kuletewa" viongozi waliokubalika ndani ya vyama vyao bila kujali wamefanya nini kwenye jamii, watafanya nini , wana uwezo gani wa kushughulika na matatizo ya jamii wala kupima uzalendo wao kwa Taifa lao

Najaribu kumfikiria nguli kama Prof. Mark Mwandosya, halafu namuangazia Dr. Salim Ahmed Salim kisha nawalinganisha hawa na Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kamanda na mtumishi wa JWTZ kisha narudi kwenye tafakuri ya nani hasa alistahili "kupewa" u Rais kwa wakati huo ndani ya hao manguli?

Tangu enzi na enzi tumekuwa tukisikia kuwa kuna kitu kinaitwa "vetting".

Kwamba viongozi wakubwa wakubwa wa nchi na taasisi mbalimbali hawawezi kuwa viongozi mpaka wawe "approved" na dawati la vetting lililojaa wakusanya taarifa za nyuma toka utotoni, za sasa na wafanya tathimini wabobezi wa uwezo wa muhusika kulingana na madaraka anayotakiwa kupewa na wabobezi wa ku "project" performance ya muhusika

Tukirejea kwenye simulizi za Mh. Balozi Polepole za hivi karibuni kabla hajatwaliwa zilizomuhusisha Mh. Mstaafu na kundi lake likiongozwa na Ndugu Azizi na tuhuma zote alizokuwa anazitoa ambazo zilipelekea ndugu Azizi kuja hadharani kuzisemea

Iliwezekanaje dawati la vetting liliweza kusema huyu ndiye mbele ya hao wengine?

Ukiniuliza mimi nitasema kuwa pengine hili dawati halina nguvu ya kuingilia siasa za vyama vya siasa vya nchi hii ndiomaana nasema vyama vina vigezo vyao ambavyo hili dawati haliruhusiwi kuvitengua?

Nadhani ni wakati sasa ili jamii ipate viongozi bora, dawati liwe na nguvu kuliko siasa za vyama

Vyama vibaki na wanachama lakini linapokuja swala la kunyofoa viongozi ndani ya hivyo vyama dawati lipewe nafasi kubwa ili kuendelea kulinda nguvu zao

Vyama vikiendelea kubaki na nguvu hizi zilizonavyo lazima vitaitawala dola. Vyama vibaki kuwa chini ya dola ili dola ibaki kuwa na nguvu ya kuvisimamia na kuviongoza kufuata mwelekeo wa nchi

Nimewakumbuka sana Prof. Mark Mwandosya na Dr. Salim Ahmed Salim
 
Salim alikuwa kichwa yule, mtu aliyeteuliwa kuwa balozi akiwa kijana mdogo sana, sio sawa na Hawa wapuuzi!

haijalishi, lkn alikuwa muslim na muslim hawaamini katika taifa, kwa muslim hakuna kitu kama taifa wala nchi bali kuna ummah, kwa mf. USA wanasema amerika first, muslim anasema ummah first, na hiyo ndiyo moja kati ya tofauti kubwa ...
 
Najaribu kumfikiria nguli kama Prof. Mark Mwandosya, halafu namuangazia Dr. Salim Ahmed Salim kisha nawalinganisha hawa na Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kamanda na mtumishi wa JWTZ kisha narudi kwenye tafakuri ya nani hasa alistahili "kupewa" u Rais kwa wakati huo ndani ya hao manguli?

JK alipewa hiyo nafasi ili kukamilisha maagano ya tambiko la Bagamoyo...

Hiyo nchi yenu sio elimu inayoamua nani awe Rais ...

Kaa vizuri na wazee wakupe soga za harakati za uhuru na maagano yake...
 
Chama kikishinda ndo kinaunda dola inawezekanaje chama kilichoshinda kiwe chini ya dola wakati chenyewe ndo kimezaa dola?
 
Tanzania na nchi nyingi za ulimwengu huu zinategemea vyama vya siasa kuzalisha viongozi wa kitaifa

Vyama vya siasa vina siasa ndani ya chama na vina siasa dhidi ya vyama vingine shindani hivyo kuna wakati kwao kipaumbele ni kuyapata madaraka pasipo kujali sana hulka, mitazamo, nguvu, wala uwezo wa huyo atakayeshika hayo madaraka

Kuna wakati kipimo chao huwa ni "nani anakubalika" zaidi kuliko wengine bila kujiuliza sana kwanini mtu huyo anakubalika na ametumia njia zipi hadi yeye kukubalika

Ndiomaa kesi za rushwa, hongo na kila aina ya ushawishi hutumika sana ndani ya vyama na hadi leo vimekosa mwarobaini kwasababu watu hutumia njia mbalimbali ili wakubalike

Jamii isiyo makini inayoendekeza siasa za vyama matokeo yake jamii hiyo itaendelea "kuletewa" viongozi waliokubalika ndani ya vyama vyao bila kujali wamefanya nini kwenye jamii, watafanya nini , wana uwezo gani wa kushughulika na matatizo ya jamii wala kupima uzalendo wao kwa Taifa lao

Najaribu kumfikiria nguli kama Prof. Mark Mwandosya, halafu namuangazia Dr. Salim Ahmed Salim kisha nawalinganisha hawa na Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kamanda na mtumishi wa JWTZ kisha narudi kwenye tafakuri ya nani hasa alistahili "kupewa" u Rais kwa wakati huo ndani ya hao manguli?

Tangu enzi na enzi tumekuwa tukisikia kuwa kuna kitu kinaitwa "vetting".

Kwamba viongozi wakubwa wakubwa wa nchi na taasisi mbalimbali hawawezi kuwa viongozi mpaka wawe "approved" na dawati la vetting lililojaa wakusanya taarifa za nyuma toka utotoni, za sasa na wafanya tathimini wabobezi wa uwezo wa muhusika kulingana na madaraka anayotakiwa kupewa na wabobezi wa ku "project" performance ya muhusika

Tukirejea kwenye simulizi za Mh. Balozi Polepole za hivi karibuni kabla hajatwaliwa zilizomuhusisha Mh. Mstaafu na kundi lake likiongozwa na Ndugu Azizi na tuhuma zote alizokuwa anazitoa ambazo zilipelekea ndugu Azizi kuja hadharani kuzisemea

Iliwezekanaje dawati la vetting liliweza kusema huyu ndiye mbele ya hao wengine?

Ukiniuliza mimi nitasema kuwa pengine hili dawati halina nguvu ya kuingilia siasa za vyama vya siasa vya nchi hii ndiomaana nasema vyama vina vigezo vyao ambavyo hili dawati haliruhusiwi kuvitengua?

Nadhani ni wakati sasa ili jamii ipate viongozi bora, dawati liwe na nguvu kuliko siasa za vyama

Vyama vibaki na wanachama lakini linapokuja swala la kunyofoa viongozi ndani ya hivyo vyama dawati lipewe nafasi kubwa ili kuendelea kulinda nguvu zao

Vyama vikiendelea kubaki na nguvu hizi zilizonavyo lazima vitaitawala dola. Vyama vibaki kuwa chini ya dola ili dola ibaki kuwa na nguvu ya kuvisimamia na kuviongoza kufuata mwelekeo wa nchi

Nimewakumbuka sana Prof. Mark Mwandosya na Dr. Salim Ahmed Salim
Walituletea kilaza akamtumalize.
 
Vetting ni porojo tu za CCM ionekane huwa kina kitu cha maana huwa wanafanya na kwamba wako serious katika kuweka viongozi.

Anayeamua nani wawe viongozi ni wenyeviti wa CCM walio madarakani wakishirikiana na waliostaafu. Nyerere ndiye aliyewaweka Mwinyi na Mkapa, Mkapa na Mwinyi walimuweka JK, JK alitaka kumweka Membe CCM wakaparuana zali likamuangukia JPM, hata hivyo mwanafunzi wake JK sasa yuko anashikilia usukani. Watakaomuweka Rais wa 2030 ni Samia na JK.
 
Anayemua nani wawe viongozi ni wenyiviti wa CCM walio madarakani wakishirikiana na waliostaafu. Nyerere ndiye aliyewaweka Mwinyi na Mkapa, Mkapa na Mwinyi walimuweka JK, JK alitaka kumweka Membe CCM wakaparuana zali likamuangukia JPM, hata hivyo mwanafunzi wake JK sasa yuko anashikilia usukani. Watakaomuweka Rais wa 2030 ni Samia na JK.
Kwa siasa za ccm hizi labda ito 2030 JK awepo pia, kama ikitokea Mungu akafanya yake kwa JK naona kabisa Samia akienda kuzidiwa kete vizuri tu iyo 2030 na pengine likamdondokea asietarajiwa.
 
Vetting ni porojo tu za CCM ionekane huwa kina kitu cha maana huwa wanafanya na kwamba wako serious katika kuweka viongozi.

Anayemua nani wawe viongozi ni wenyeviti wa CCM walio madarakani wakishirikiana na waliostaafu. Nyerere ndiye aliyewaweka Mwinyi na Mkapa, Mkapa na Mwinyi walimuweka JK, JK alitaka kumweka Membe CCM wakaparuana zali likamuangukia JPM, hata hivyo mwanafunzi wake JK sasa yuko anashikilia usukani. Watakaomuweka Rais wa 2030 ni Samia na JK.
Hizo porojo kwenye vetting ndo zinatakiwa kuondoka ili tupate viongozi bora na sio bora viongozi
 
Vetting ni porojo tu za CCM ionekane huwa kina kitu cha maana huwa wanafanya na kwamba wako serious katika kuweka viongozi.

Anayeamua nani wawe viongozi ni wenyeviti wa CCM walio madarakani wakishirikiana na waliostaafu. Nyerere ndiye aliyewaweka Mwinyi na Mkapa, Mkapa na Mwinyi walimuweka JK, JK alitaka kumweka Membe CCM wakaparuana zali likamuangukia JPM, hata hivyo mwanafunzi wake JK sasa yuko anashikilia usukani. Watakaomuweka Rais wa 2030 ni Samia na JK.
Sio kweli hata kidogo Nyerere hakumtaka Mwinyi kabisa
 
Back
Top Bottom