Siasa na Uwendawazimu Jf

Sanchor

Member
Nov 15, 2013
11
0
Nkiwa ningali mdogo nlipenda siasa sana kiasi kwamba nliapa nikiwa mkubwa lazima niwe mwanasiasa. Labda hii ilitokana na babu yangu ambae alikua mmoja wa wanasiasa wakongwe (jina linahifadhiwa msije mkaniuliza picha) kupitia chama tawala na amefanya kazi kubwa ya kujenga nchi hii kabla ya kuamua kustaafu kwa hiari. Simulizi zake kwa jinsi alivyokua akipenda kutenda haki zilinipa hamasa sana. Kwa kweli nlifarijika sana.
Lakini baada ya kuanza kujielewa hali ya kupenda siasa ilianza kubadilika kwa kuona uhalisia wa siasa tofauti na zile hekaya za mzee wangu.
Nakumbuka Bukoba katika kipindi cha uchaguzi 2005 nlijitahidi kuhudhuria mikutano ya hadhara ya Balozi Kagasheki na Lwakatere. Kwa kua nlikua nikisoma na watoto wa ndugu wa Lwakatare nlimfurahia sana Lwakatare achukue kiti ijapokua nlikua sijafikisha umri wa kupiga kura.
Ila nlichokishuhudia katika kampeni za Lwakatare ilikua ni matusi na kejeli kwa Kagasheki. Roho iliniuma sana ukizingatia kua Kagasheki alikua anaendesha siasa safi bila matusi labda kwa mazoea kwamba alikua amezoea siasa safi akiwa balozi.
Hali hiyo ilibadilika ghafla nadhani ndugu Kagasheki alichoka kwa kashfa na dharau naye akaamua kujibu mapigo.
Katika chaguzi ndogo jijini Arusha 2013 siasa za matusi ndo ilikua order of the day. Kampein za CCM zilijaa matusi kwa mh. Lema utadhani yeye ndo alikua anagombea udiwani.
Bila kupepesa macho hali hiyo ndo iko humu jf. Watu humu ndani wanatoa matusi mazito na dharau. Sidhani kama ndo siasa safi aliyotufunza muasisi wa taifa hili.
Bila kuangalia hoja mtu anapinga ilhali tu kapinga alafu haohao ndo wanalilia demokrasia. Kejeli za kutaka ushahidi wa picha kushindana elimu ndo order humu ndani.
Elimu si kigezo cha kutoa hoja nzuri ila inasaidia kuweza kutoa hoja. Cha kushangaza kwa dharau hizo cjui wanaonesha mpaka majumbani kwao kwa wazee wao wasiokua na degree! Wanakashifu kila mtu mwenye mawazo kinzani. Wako tayari kufa kwa kutetea hoja ata kama ushahidi unaonesha kua ZZK au Mbowe au CCM wanamakosa.
Elimu si kutusi mtu bali kuheshimu.
Haya yate ni madhara ya kuchanganya siasa katika kila hatua ya maisha
 

Nebuchadnezzar

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
212
195
Ishi kwenye mazingira kulingana na mazingira yenyewe yanavyoruhusu.

Ukikaa na mtoto hauwezi kuongea/kupiga naye story kama unapokuwa na mkubwa mwenzako. Binadamu aliyekamilika ni lazima awe na uwezo wa kubadilika kulingana na mazingira.

Mtu akikuletea ubabe na wewe kuwa mbabe, akiwa mstaarabu na wewe kuwa mstaarabu.

Kuna baadhi ya watu wamestaarabika hapa Jukwaani kwa mfano Watu8 na wengine ambao wanajifanya wamewehuka kama Matola. Hao wanaojifanya wamewehuka wala wasikuumize kichwa akiingia kwenye kumi na nane zako mpe kubwa ila ujiandae kwa :ban:.

You only live once.
 

my web

JF-Expert Member
Dec 23, 2012
1,593
0
humu tatizo vijana wa bavicha kina mtoi.molemo.ben sa8.mungi wakisha piga viroba basi matusi kama kawa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom