Siasa na Maisha

Siasa na Maisha

Joined
Jul 26, 2022
Posts
14
Reaction score
10
Je ni kweli siasa za Tanzania zimepoteza mvuto na ushawishi kiasi kwamba wananchi wameona siasa hazina maana na badala yake wameona wawe mashabiki wa mpira?

Itakuwa ni kichekesho kwa raia wa Tanzania kutozingatia siasa ambazo ndizo zinazoamua maisha yao na kuona mpira una maana sana kwenye maisha yao?

Baadhi ha wasomi wanaona mwelekeo wa wananchi ulivyo sasa yaani kutofuatilia mambo ya msingi na kufuatilia mambo ya ovyo kama udaku na mpira ni ishara kwamba Tanzania haina national conciousness kwa sababu taifa halikuwaandaa wananchi wake kifikra bali kuwa wajinga.

Huwezi amini hata vyombo vya habari siku hizi vinaweka attention kubwa sana kwenye udaku na mipira kuliko mambo ya msingi. Mambo ya msingi hupewa airtime ndogo sana kwenye media. Sasa sijui ni makusudi au vipi?

Leo hii mtu kama Manara anapewa airtime kubwa tena kwa mambo ya kipumbavu kabisa atakayozungumza lakini mtu kama Bashe au Mbowe au Shivji hawapewi airtime na vyombo vya habari mpaka unashangaa why watu ambao wanaweza kusema mambo muhimu wanawekwa kando halafu nyombo vya habari vinatoa attention kwa waendeleza ujinga?

Wengine wanasema mfumo wa elimu ndio umepelekea kuwa na taifa la wajinga na wasiojipambanua.

Je, wewe mdau unasemaje?


FB_IMG_16589947285917090.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom