Siasa na hamasa ya madaraka katika kuwatumikia wananchi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Toka tupate uhuru ni zaidi ya miaka 58 imepita,nchi yetu imepitia vipindi na mifumo mbali mbali ya uendeshaji serikali kupitia serikali ya CCM.

hatimaye mwaka 1992 tukaingia Katika mfumo wa vyama vingi kutokana na mabadiliko makubwa ya mwenendo wa siasa za kidunia.

Taifa letu limepita vipindi vingi vya mpito katika utekelezaji wa sera vinavyo ongozwa na CCM.

KIMANTIKI utaona kuwa CCM ina uzoefu mkubwa kisiasa kuliko vyama vingine vya upinzani.

Lakini unapo itafakari CCM na serikali inazo ziongoza toka tupate uhuru kwa kubadilishana marais lazima utajiuliza mambo mengi.

Lakini kubwa ni kushindwa kusimama kama chama cha ukombozi kilichoongoza nchi kwa miaka zaidi ya 58,kwa aina ya mwenendo wa usimamizi wa serikali mwaka hadi mwaka.

Hali inayo kifanya chama kutoka kuwa chama cha siasa na kuwa chama dola, kinachotegemea nguvu ya dola kuliko itifaki, itikadi na falsafa ya chama kinacho simamia msingi ya haki na usawa.

Hali hii ina athiri kwa kiwango kikubwa maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa taifa pia.

Kwa kuwa kila atayekwenda kinyume na CCM na serikali yake anaonekana adui wa Taifa, na atashughulikiwa kwa nguvu zote kumdhoofisha kiuchumi, kijamii na kisiasa pia.

Mathalani wapo walifilisiwa mali zao na kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi kwa kuwa wanakosoa utawala huu,usio amini kwenye misingi ya majadiliano.

Athari hizi zina wagusa wananchi moja kwa moja, na kwa kuwa wamejengewa hofu, wamekosa uhalali wa kuikosoa na kuihoji serikali waliyo ipa mamlaka na madaraka ya kuongoza.

Kwa athari hii tunaona aina ya watawala wanao jenga hofu kwa watawaliwa, na kutengeneza sheria kandamizi zinazo pora haki ya kujadili, kukemea udhalimu na mwenendo mbovu wa ukandamizaji kwa wananchi walio iweka madarakani.

Matokeo yake watu wanaamua kujisalimisha CCM kulinda maslahi yao.

Hii ni sawa na kuchonga kinyago chako kisha ukiweke sebuleni then kinyago hicho hicho kikutie hofu usiingie chumbani wala kupaza sauti ndani ya nyumba yako.

Abraham Lincoln amesema "Those who deny freedom to others deserve it not for themselves"

Wale wanaozuia uhuru kwa wenzao nao pia hawako huru pia.

Kwa kulitambua hili Abraham Lincoln ameliona hili kwenye political and inspiration na ndicho tunacho kiishi.

Kwa hofu hii si kwamba CCM wako salama, ndiyo maana hawataki mawazo mbadala, hawako salama ndiyo maana wameikabidhi siasa kwenye vyombo vya dola ili kuweza kudhibiti ushindani wa kisiasa utokanao na nguvu ya hoja ya vyama mbadala katika mizania ya siasa za vyama vingi na walio na mtazamo unao kinzana na watawala.

Na kwa kuwa siasa ya Tanzania imegeuzwa Vita maendeleo yatabaki kuwa ndoto.

Tumeona miradi mikubwa inayo gharimu fedha nyingi na kupandisha deni la taifa kila kukicha ina kwama kwa kuwa hatukuwa na mipango kazi, serikali ikadhani kukandamiza demokrasia nchini italeta tija na maendeleo ya haraka.

Demokrasia na maendeleo ni vitu viwili mapacha kila kimoja kikichochea uimara wa mwenzake.

Unapo zuia mawazo mbadala ukijiona uko sawa una finya wigo mpana wa majadiliano ya kujiletea maendeleo.

Watawala wetu wamekuwa wakisema Tanzania Tuna demokrasia yetu, lakini toka kuanza kutumika kwa demokrasia hiyo inayo nadiwa na CCM, maendeleo nayo yamekwama.

Demokrasia ipi inayo dumisha rushwa ya madaraka, ukitoka upinzani tutakupa U- DC ,RC, DED, n.k

Demokrasia ya kubagua wenye haki na wasio na haki ndani ya nchi moja, haki ya kuwa mwanachama wa CCM tu bila kuwa na upinzani tukidhani tuko salama.

Kwa kulitambua hilo ndiyo maana ikitokea mtu akakwamisha misaada, kama alivyofanya Zitto atalaaniwa na kutishiwa uhai wa maisha yake, kwa kuwa tume plan kushindwa kabla mkakati wa kujikwamua kwa kuwa tume ruhusu dola kusimamia siasa,kwa kuzuia mawazo mbadala.

Hata mawazo na mikakati ya siasa za kidola zina shindwa kuleta maendeleo kwa kuwa hazina plan B zaidi ya kutumia maguvu yasiyo na tija kwa taifa.

MATOKEO yake:

Serikali kujiona yenyewe ndiyo bunge, serikali na mahakama, hali inayozua utata mkubwa wa mgawanyo wa madaraka na mipaka ya utendaji.

Hali inayoathiri usimamizi na utungaji wa sheria kwa kuwa mfumo una uhisha batili dhidi ya haki na kuibua tabaka la watawaliwa dhidi ya watawala.

Ndiyo maana leo ukisema tume huru ya uchaguzi na #katibampya ni sawa na kutengua fumbo la imani.

Utashambuliwa na watawala kwa kuwa utashi wao ni kutumia madaraka yao kuimarisha himaya zao binafsi.

Kwa kuwa baadhi ya Watanzania ambao ni wanasiasa hasa wa upinzani wameipokea hofu, wamejitazama binafsi kuliko ilivyokuwa dhamira yao kwa maslahi ya familia zao, wameamua kujificha kwenye chaka la wanao Ng'ang'ania madaraka ili kukidhi malengo binafsi.

Kwa muktadha huo tutegemee wimbi la walioficha dhamira zao wakiwa upinzani, wakiamini watavuka salama, lakini wakiona nusura bado iko mbali hasa 2020 makundi kwa makundi yataingia CCM.

Pamoja na CCM kupoteza legitimacy ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi nao hawako salama, kwa kuwa wamekubali kutoka kwenye misingi ya haki na usawa na kukumbatia siasa za chuki na visasi tutegeme anguko kubwa la amani nchini.

Pamoja na kimbilio la wanyonge wenye nia na hamasa ya madaraka hali ya CCM si shwari, utamaduni na falsafa ya majadiliano imepokonywa na kikundi cha wachache wanao pambana kutengeneza mtandao ndani ya chama, watakao hodhi nguvu na mamlaka ya chama.

Ndiyo maana wanaokosa fursa za kuongea ndani ya vikao kwa kuwa fikra Sahihi za Mwenyekiti zinadumishwa, wameamua kutoka nje kuzungumza kwa kutumia mitandao ya kijamii, japo wana shughulikiwa kwa nguvu ya dola.

UPINZANI NAKO SI SHWARI

Unapokuwa kuwa na chama dhaifu kinacho ongoza serikali, msipokuwa makini mtakuwa na vyama vya upinzani babaifu.

Kwa kuwa udhaifu wa chama tawala huvifanya vyama mbadala kubweteka bila kufanya mikakati madhubuti yenye kuleta ushindani wa kisera wenye tija.

Tunajua nguvu kubwa ya dola inavyo saidia CCM kudhoofisha nguvu ya upinzani bado vyama hivi vina nafasi kubwa ya kuonyesha nia yao ya kuongoza dola kwa kunadi sera mbadala kuliko kuhangaika kuwaelezea wahamaji.

Tumeona mapambano ya nje ya nchi kwa kutumia jukwaa hilo kusaka haki, lakini juhudi hizi zimechelewa kuanza.

Kuchelewa kuanza harakati hizi za ukombozi kipindi hiki, kina vifanya vyama hivi kuwa vya kipindi cha uchaguzi tu, hali inayo ondoa kuaminika kwa wananchi na ukizingatia mkakati wa wahamiaji unavyo kuwa kwa kasi.

Kwa hali ya siasa za sasa za Tanzania maridhiano hayana tija kwa kuwa aliyeshika mpini ana tumia lugha hiyo kama udhaifu wa upinzani.

Kwa kuwa vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria, zuio lolote linalo pingana na sheria na kanuni ya uanzishwaji wa vyama vya siasa ni batili, kuendelea kujificha nyuma ya zuio hilo ni udhaifu mkubwa na ushindi kwa CCM.

Migogoro isiyo na tija na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma bila justification inayoeleweka haivisaidii vyama hivi.

Mnachokihubiri ndicho mnachopaswa kukisimamia, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "mke wa mfalme hapaswi kutuhumiwa na tuhuma ovu " mkiruhusu tuhuma zikasemwa bila ufafanuzi mnaji dhoofisha wenyewe.

Watanzania wanataka mbadala wa serikali hii iliyo wachoka Watanzania. Mkisimama imara Tanzania itasimama nanyi.

Wimbi la wahamaji ambao hawana impress na community zaidi ya kusaka mkate wa family zao usiwatoe kwenye mataruma ya reli, kwa kuwa kwenye msafara wa mamba, kenge nao wamo.
 
BARUA KWA MHESHIMIWA RAIS:

WATEULE WAKO WA MKOA WA MOROGORO NA WILAYA YA KILOSA WAMEWEKWA MFUKONI NA MFANYABIASHARA WA DUMILA ANAYEITWA SHABANI MNYINGI.

MHESHIMIWA Rais,ninayoheshima kubwa kukuandikia barua hii kwa masikitiko makubwa,
Hii inatokana na kuona shida waipatayo wananchi wa wilaya ya kilosa,hususan kata za kitete,mbigiri,msiwero na dumila.

Hivi karibuni uliituma tume ya maridhiano kwenda kusikiliza kero za wananchi mkoani humo hasa kwenye maeneo yenye matatizo ya ardhi yasiyoisha. Tume ilikusanya kero,kilichoshangaza wengi ni baada ya mfugaji anaitwa lenjeka kueleza kuwa, mashamba yao pia yamechukuliwa na Mh Anna Malinda
Mh Lukuvi na viongozi wengine wakubwa

Hii inaonesha ndiyo sababu ya ugumu wa utatuzi wa migogoro ya maeneo hayo,kwakuwa wakubwa wasiotosheka na walichokivuna wakiwa madarakani au wanachokivuna hata Sasa wakiwemo madarakani kutaka kujilimbikizi utajiri kwa kuwazurumu wanyonge kwakutumia madaraka yao.

Wakubwa Hawa wanamtumia mfanyabiashara wa dumila anayeitwa shabani mnyingi au Kelvin mnyingi na Afisa tarafa ndugu nchimbi
Mtu huyo alimepora mashamba mengi Sana ya wananchi wakishirikiana na wakubwa wa wilayani na mkoani.

Hakuna anayemgusa kwa neno lolote.
Mwaka Jana mwishoni,wananchi walilalamika kwa mkuu wa mkoa,ikaonekana huyu mfanyabiashara asimamishwe kutumia mashamba hayo.

Mfanyabiashara huyo hivi juzi juzi alienda huko mashambani na kuwatishia watu kuwa atawapiga risasi na akatamba kuwa siku ya pili yatafuat mabomu huko mashambani.
Juzi ameanza kuyalima mashamba hayo usiku,taarifa zilipopelekwa kwa viongozi kuanzia Afisa tarafa,wilaya na mkoa,hakuna anayemchukulia hatua mfanyabiasha huyo.

Mfanyabiashara huyo anatamba mbele za watu kuwa hakuna wa kumfanya chochote,kwakuwa hata mkurugenzi wa wilaya anamdai fedha zake nyingi Sana.
Na kuhusu polisi,ameshapiga simu kwa OCD na Rpc na kuwapa taarifa kuwa wasitume Askari kumkamata Bali wampigie simu atakwenda mwenyewe kituoni.

Mh Rais, kwa mamlaka uliyopewa na wananchi,wasaidie wananchi wa wilaya hiyo hususan kata hizo.
Kama hawa wakubwa wanamtumia mfanyabiashara huyo kuzurumu maeneo ya walala hoi ni kiongozi gani atakayemgusa mfanyabiashara huyo?
NI WEWE TU MKUU WA NCHI UNAWEZA .

Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya wote hawamuwezi.
Afisa tarafa,huyo ndiye rafiki yake mkubwa anayepanga nae mipango ya kupora mashamba.
Suala hili katibu wako CCM taifa,amelishindwa na mfanyabiashara huyo amemshindwa.

Hakuna kikao au mkutano wa utatuzi wa migogoro ya maeneo hayo, asiyotajwa mfanyabiashara huyo na rafiki yake Afisa Tarafa ndugu nchimbi,kuwazurumu wananchi na kuwanyanyasa.
Hawa wamekuwa tishio sana,polisi wote hawana meno kwa Hawa watu wawili,wanafanya jinai nyingi tu na kwa wazi,lakini polisi wanaangalia tu.

Kama unapita humu MHESHIMIWA taarifa ndiyo hii. Watu wengi wanyonge wanateseka na kuzurumiwa na wakubwa wachache wenye tamaa ya Mali ambao hawatosheki na walivyonavyo.
NAWASILISHA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa ndo ilivyo siasa ni biashara na maslahi ya vikundi ukiingia kwenye biashara ya siasa au kikundi cha siasa haya lazima utayakuta..
katika maisha usitegemee eti mtu akutegenezee mteremko uwe unakula kuilaini laini..
Wengi hujali mashali binasfi kwanza hata kama atachelewa kuyapata lakini atatengeneza mbinu zimfikishe katika lengo lake iwe kwa kupitia huu wimbo siasa ni maisha .
Na kwa kufahamu zaid katika vikundi hivi vya siasa au hii biashara ya kisiasa kati ya watu milion 50 waamuzi wa mambo hawazidi 2000 wanaojiitaga kamati kuu.
Kwa maana hiyo walalamishi na wapongezaji watazidi kuwepo tu,
Mwenye kukosa alalama,na mwenye kupata atapongeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom