Siasa Mashule au msajili mpaka akurupushwe

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,941
900
IMG_0036.JPG

Na Edwin Moshi wa

Globu ya Jamii, Makete

Umoja wawanawake wa CCM Tanzania (UWT) umeahidi kutoa solar Panel moja yenyethamani ya zaidi ya tsh laki nane kwa shule ya sekondari Ikuwo iliyopo wilayaniMakete mkoani Njombe
Ahadi hiyoimetolewa na Naibu katibu mkuu wa UWT Taifa Eva Kihwele wakati alipofanya ziarakatika shule hiyo jana ambapo pamoja na mambo mengine alikagua mabweni yawasichana yaliyopo shuleni hapo
Akisomewataarifa ya shule hiyo na Mkuu wa shule alisema pamoja na mafanikio lakini wanaupungufu wa sola kwa ajili ya kutoa nishati ya umeme ambayo itawasaidiakuongeza ufanisi na utendaji kazi shuleni hapo ikiwemo kujisomea jambolililoigusa UWT na kuamua kutoa msaada huo, Mbali na kuahidi kutoa sola hiyo, pia kiongozihuyo ametoa shilingi laki moja kwa ajili ya sukari ya wanafunzi hao ambaowanalala shuleni hapo

Akizungumzana wanafunzi hao Naibu Katibu mkuu UWT Taifa Bi Kihwele amewataka kuzingatiamasomo kwa kuwa watoto wengi wa kike wamekuwa hawafikii malengo yao, nakuwataka wao kuwa mfano wa kuigwa kwa kusoma kwa bidii hadi wafikie chuo kikuu,ili badae wawe na kazi nzuri itakayowasaidia kuingiza kipato chao cha kila siku
Viongozi wakitaifa wa UWT wapo wilayani makete kwa siku tatu kufanya shughuli mbalimbaliikiwemo kukagua miradi ya maendeleo na kuchukua changamoto mbalimbali zawananchi ili kuzipatia ufumbuzi



 
Back
Top Bottom