Siasa kuingilia soko la mazao ya kilimo-hii ikoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa kuingilia soko la mazao ya kilimo-hii ikoje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndamwe, Jan 20, 2010.

 1. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele kwa wana JF wote!

  Kumekuwepo tabia ya wanasiasa kadhaa hususani wakuu wa wilaya nk kupiga marifuku uuzaji wa mazao ya kilimo katika masoko yanayotokea kwa kisingizio cha usalama wa chakula kwa eneo au wilaya husika. Mara nyingi mazao ya wakulima vijijini yana bei ndogo sana kiasi cha kuwaumiza wakulima na kuzidisha umaskini. Hivi miezi ya karibuni palikuwa limejitokeza soko zuri la ndizi za Kagera likiwa kule mpakani na Uganda, na wakulima walikuwa angalau wanafurahi kwamba ndizi zilizokosa soko la uhakika kwa miaka mingi sasa tatizo hili lilikuwa limepata mkombozi. Ni mengi, pia hata kahawa pia wakulima wamekuwa wakikatazwa kuuza Uganda kwa muda mrefu ambako waganda hununua kwa bei angalau ya kuridhisha na malipo ya papo kwa papo.
  Inapotokea wanasiasa wakapiga marufuku ya soko la ndizi mimi napata kichefuchefu kwa sababu:
  Kwanza anayehusika na usalama wa chakula ni mkuu wa kaya husika
  Pili, serikali haimpatii mkulima pembejeo za kilimo,
  tatu, wanasiasa hawagharamii elimu ya wakulima maskini na matibabu yao,
  nne, wanasiasa wanasumbua sana wakulima hao hao na michango isiyokwisha,
  tano, wanatueleza kuwa hizi ni zama za uchumi huria-wa ushindani
  n.k.

  Sasa hii imekaaje? naona kama inarudisha moyo wa watu kuzalisha zaidi kwa maana ya kutokuwepo soko la uhakika la mazao yao.
  WanaJF wenzangu tutawasaidiaje hawa wakulima maskini wa Tanzania kwa tabia hii?
  Nawasilisha kwa heshima.
   
Loading...