mafimboo
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 2,415
- 978
Kimsingi elimu ya kitanzania ni moja ya elimu isiyofaa katika dunia ya leo, mfumo wa elimu ya tanzania umeunganishwa na siasa na kujichimbia katika siasa,jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa elimu yetu elimu inapaswa kuamua nini inataka na sio wanasiasa wanataka nini katika elimu.
Tumeshuhudia miaka ya hivi karibuni wanasiasa wakichezea uhai wa taifa ambao ni elimu kwa maagizo ya ajabu ajabu wanayobuni kwenye vichwa vyao,na kwasababu katiba inawaruusu basi ndoto zao zinatekelezwa katika elimu,lakini hawawajibiki na wala katiba haiwawajibishi mifumo walioibuni inapokwama. Mfano yuko bwana mmoja aliamua kuunganisha fizikia na kemia na wazo lake likakubalika likatekelezwa,baadaye wakailfuta,baadae wakaja wachache wakafuta mchujo wa kidato cha pili kisha wakaja wengine wakarudisha ,wakaja wengine wakaanzisha shule za kata ,shule zikiwa na madarasa mawili bila maabara,zikaenda hivyo hivyo hazijakamilika mpaka leo hazijakamilika,ghafla waziri mmoja katika awamu ya nne akatangaza kufuta ada za mitihani ya taifa za kidato cha pili na nne,haikuchukua muda walipoona maji ya shingo wakairudisha shapu, wakaja wengine wakafuta mfumo katika divisheni wakaleta mfumo katika grade za G.P.A ,haijachukua muda akaja jemadari na mama mtaalamu wa maelimu wakafuta mfumo wa matokeo katika G.P.A kwenda katika mfumo wa zamani wa Divisheni ,huyu mama waziri aliyeteuliwa na jemadari jiwe akaenda mbali zaidi akapandisha madaraja ya kwenda vyuo,akapandisha G.P.A za kwenda chuo kutoka G.P.A 2.9 mpaka G.P.A 3.5 kwa wenye Diploma ghafla alipoona maji ya shingo na vyuo vitakosa watu akashusha G.P.A kutoka 3.5 mpaka 3.0 za kuingilia chuo, na vijana wa form six akapandisha kutoka E E mpaka DD kwenye kombinesheni,jemadari akatangaza kufuta michango yote katika elimu,na sasa elimu inatolewa bure,japo ni wazi sasa kutoka katika taarifa za CA elimu bure sasa ni maji ya shingo,jemadari a kakaza buti na kusukumia maji ya shingo kwa wasio na hatia
Kwa maigizo haya tuandike tumeumia katika elimu,ktk maigizo yote hakuna aliyeijaribu kugusa content/mifumo ya elimu yetu kama inastahili na inakwenda na wakati ,Tafakari?