Siasa inavyotuathiri Watanzania

Siasa inavyotuathiri Watanzania

LuciusKaisery

Member
Joined
Feb 19, 2018
Posts
18
Reaction score
31
Siasa ina-athiri maisha yetu ya kila siku. Viongozi serikalini wananasiasa ndio wanafanya maamuzi ya nchi kwa niaba yetu.Kiasi cha kodi unacho lipa, aina ya elimu unayosoma, mshahara unaolipwa yote haya yaliamuliwa na kiongozi ambae ni mwanasiasa.

Tupo kwenye maombelezo ya Aquilina .B. Akwilini huyu ni mwanafunzi amepigwa risasi na polisi. Huenda hakuwa mfuasi wa siasa au mkereketwa wa siasa na pia hakuwa kwenye shughuli za kisiasa lakini kapoteza maisha yake tokana na siasa.

Siasa na mifumo yake huathiri kila mwananchi nchini uwe mkereketwa au usiwe mkereketwa ama uwe mfuasi au usiwe mfuasi, siasa huathiri maisha yetu na jamii zetu kwa ujumla.

Siasa ina-athiri nyanja zipi?

Mifumo na mitahara ya elimu nchini ni duni tokana na siasa zetu,Uchumi wetu ni duni tokana na siasa zetu, Huduma za Afya nchini ni mbovu ni tokana na siasa zetu, Kuna sera mbovu na sheria mbovu ni tokana na siasa zetu, Tunalipa kodi kubwa na zisizo za msingi ni tokana na siasa, Demokrasia inaminywa tokana na siasa zetu, Vyombo vya habari vinafungwa bila sababu tokana na siasa zetu, mishahara ya wafanyakazi nchini ni duni tokana na siasa zetu n.k


Kwa nini tunasema siasa?
Viongozi hupatikana kupitia uchaguzi, kitendo cha kupiga kura, kufanya kampeni au kugombea hiyo ni siasa tayari.

Viongozi serikalini au wabunge ndio hufanya maamuzi ya nchi na maamuzi hayo yanaweza kuwa ya kunufaisha taifa au kudidimiza wananchi na taifa au kutetetea maslahi ya chama au viongozi wenyewe.

Viongozi ndio huunda sera na sheria, Viongozi ndio hao husimamia sera na sheria hizi.

Viongozi hupelekea kuwepo kwa demokrasia au kutokuwepo, viongozi hupelekea kuwepo kwa amani nchini au kusiwepo.

Kwa mantiki fupi uwepo wa viongozi wabovu hupelekea kupata sera na sheria duni nchini, serikali mbovu kama serikali ya awamu ya nne n.k, na viongozi wabovu hupatikana na siasa mbovu.






MIFUMO YA SIASA NCHINI.

Vyombo vya habari nchini vinafanya kazi kwa uoga sana kuhofia serikali iliyopo madarakani maanake mifumo ya siasa nchini ni duni inaminya demokrasia ya taasisi hizi kufanya kazi inavyotakiwa. Lakini taasisi sisi au waandishi wa habari wanaathirika kwa namna nyingine huenda wengine hawajajikita kwenye siasa. Mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Azory haonekani hadi leo moja kwa moja kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini tunahaki ya kulaani mifumo ya siasa nchini.

Vifo, mauaji, kupotea kwa watu na Utekekaji, Toka serikali awamu ya tano ianze mhuhura wake haya mambo yamekuwa kawaida sana na tukifanya takwimu tutakuta ndani ya awamu ya tano yamekuwa kawaida sana. Serikali imetoa msaada gani? Imetoa ripoti ya uchunguzi kuwa imefikia wapi? Hakuna mtanzania anaweza akahoji ni tokana na mifumo ya siasa zetu. Ukizungumzia serikali kwa kuikosoa usalama wako uko rehani unaweza kutekwa au kupotea katika mazingira ya kutatanisha au kuuliwa na watu wasiojulikana.



Uminywaji wa demokrasia nchini. Hamna Uhuru wa kujieleza, haki ya maandamano, uchaguzi huru na wa haki, uhuru wa vyombo vya habari ukiangalia hizi ni haki za kikatiba lakini haki hizi zinaminywa na serikali na tokana na uwepo wa mifumo duni ya siasa nchini huwezi kwenda kudai haki na ukienda kudai unaweza usipewe.

Mifumo ya ELIMU NCHINI.
Tumesoma au tunasoma au tulisoma na watoto wetu wanasoma elimu duni tokana na viongozi wetu wa kisiasa tunawapa nyadhifa za kusimamia na kukuza elimu nchini. Hakuna anaeweza kukuza au kubadilisha mifumo ya elimu nchini bali wanawaza kubadilisha PASS MARK. Elimu yetu ni BOOKISH EDUCATION na ni THERORITICALLY ORIENTED inatuandaa kujibu mitihani na kutupatia mentality ya kuajiriwa. Yote haya yanatokana na siasa zetu nchini.

Bungeni
Wabunge wa CCM kuungana na wabunge wa vyama pinzani kuunga mkono au kupitisha hoja hata iwe msingi kiasi gani au manufaa kwa taifa itapingwa si kwamba hoja ni mbaya bali ni kwa sababu mtoa hoja sio mwana-CCM.

Kodi nchini (Kiasi cha kodi, aina ya kodi, mifumo ya kodi.)
Kiasi cha kodi tunacholipa, aina ya kodi na mifuo ya kodi maamuzi yote kuhusiana na yote hayo yameamuliwa na mwanasiasa tuliyemchagua sisi. Mifumo duni ya kodi inasababishwa na aina ya viongozi tunaowachagua.



Ushauri.
Ewe mtanzania unasema hushiriki kwenye shughuli yote ya siasa iwe kupiga kura huenda ulikuwa hujui siasa inavyoathiri maisha na jamii yako kwa ujumala. Mitazamo ya kusema unauhakika wa kula,watoto wako wana uhakika wa kwenda shule na kulala huna haja ya kushiriki kwenye siasa wewe ni miongoni wa kusasababisha uwepo wa serikali mbovu na mifumo duni ya siasa. Nadhani huu ni wakati wa kufanya na kushiriki siasa zenye manufaa kwa taifa letu.
 
Swali: Hivi nani anastahili kuwa kiongozi wa nchi ili siasa hizi ziende sawa sawia
 
Sema wapinzani wakija choka mbona tutakua wakimbizi mm tangu 2015 ctaki siasa maana niliona ni kuumiza hakiri tu maana bado hatuajakomaa kua na wanasiasa wanaopingana kwa hoja ila Bali ni minguvu na ubabe
 
Back
Top Bottom