zipompa
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 12,485
- 27,620
Salamu wakuu,
Wiki 2-3 nipo katavi kwa shughuli za utafutaji. Nimekuwa mwenyeji mji huu sasa kitu kinacho kera ni wananchi kuendekeza siasa hata katika mambo ya msingi.
Kuna askari mmoja anasimamia sheria ipasavyo hachukui rushwa wala kuwa na upendeleo pindi akiwa kazini.
Nilipata sifa za huyu bwana baada ya kuwa na safari zangu vijijini kutafuta mzigo, kila boda nae mchukua lazima anipe habari za askari huyo na kuhofia kama akitukamata lazima pesa itutoke (kosa la kofia ngumu, bima, mavazi yasiyo stahiki n.K)
Katika mazungumzo na bodaboda wamefanya jitihada zote kumuondoa ikiwa ni pamoja na kupeleka malalamiko sehemu mbalimbali (ccm mkoa ila wakiombwa udhibitisho wa tuhuma hawana), vikao vya wazi wakitamka wazi hawamtaki wakiulizwa sababu hawana ni kwa kuwa tu anasimamania sheria.
Kilicho nisikitisha ni juzi nilikua na wafanyabishara flani wakipanga kumuondoa mtu mwingine, kisa nae anasimamia sheria. Hii ilinifanya nihudhurie mkutano wa kumuondoa huyu bwana. Nilicho kisikia kikanisikitisha sana.
Huyu bwana ni afisa ushirika wilaya, kumekuwepo na kilio cha tumbaku nchi nzima juu ya kuzidi kwa uzalishaji.
Uchunguzi wa tume ya mkuu wa mkoa katavi, ulionesha wafanya biashara kwa kushirikiana na wakulima waliingiza tumbaku toka nje ya mkoa hivyo kufanya uwepo wa zidio la uzalishaji.
Tume ikapendekeza malipo ya 40% kwa wakulima walio uza tumbaku awamu ya kwanza, afisa ushirika akapinga na kushauri walipwe 80% na baki ya 20% walipwe baada ya wenzao kuuza tumbaku uliyo baki.
Tumbaku iliyo baki iliuzwa kwa bei mbaya, madeni yamekuwa mengi kuliko mapato hivyo kurudisha 20% imekuwa ngumu.
Huyu afisa akashauri wapewe 11% na 9 inayo baki walipwe hawa walio uza kwa bei mbaya. (hapa ndio mgogoro)
Walioingiza tumbaku kwa magendo wanafahamika na ndo hawa wanaongoza afisa huyu atoke kwa kuwa ajawapa 20% ameshauri wapewe 11%
Nilicho cheka na kukumbuka tukio la yule afisa wa polisi ni pale hawa wafanyabiashara kwenda ofisi ya ccm kudai afisa aondolewe. Wakiulizwa sababu hawana hoja.
Huu mkoa unanishangaza sana, jambo la kujenga hoja wao wanakimbilia ofisi za ccm kutaka flani aondolewe.