SIASA: Hapa Nani Mjinga?

SIASA: Hapa Nani Mjinga?

Joined
Jul 28, 2013
Posts
72
Reaction score
17
Siku nimekuwa nikijiuliza njia kuu mbili za kuwa chagua viongozi wa siasa kupitia vyama vyao. Mambo makuu yafuatayo huwa najiuliza likiwemo kuwa " sisi wananchi ndiyo wajinga au wanasiasa ni wajinga" siasa zao hazipimiki kwa Jamii yenye uelewa katika mambo ya maisha ya kawaida ya wananchi.

1. wanasiasa wetu kujipa uwezo mkubwa wa kutenda kuliko uhalisia wenyewe.. nikiingia ikulu, nikiwa mbuge, diwani, m/kiti wenu , mtapata maji bure, shule nitawaletea madawati, nitafanya hili na hili,....!? Yote hayo tunaambiwa bila kujiuliza mtaji atatoa wapi!? Na kweli yanawezekana kutekelezeka kwa kiwango anachodai!? Mkimchagua anaanza kuwa na kigugumizi..., utekelezaji zero, maneno mengi...

2. Je, tunapata muda wa kuwapima uwezo wa viongozi wetu au tunapelekwa na mkumbo wa vyama? katika kushabikia chama badala ya hoja na uwezo au sifa za kiongozi wa chama husika, tumepata viongozi ambao wamepitishwa kwa mkumbo tu wa chama, hawanasifa ya uongozi, na pengine hawanauelewa wa mambo au elimu ya uraia, kitu ambocho ni cha msingi kabisa kwa wanasiasa. Madhara yake ni kupandikiza migogoro katika jamii bila kujua au kwa makusudi kabisa. Hawa hata uelewa wa sheria za nchi kwa ujumla wake!

3. Viongozi wetu kwa dhati kabisa wanawatumia wananchi kama ndiyo fimbo yao ya kujipatia mawindo. Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu vurugu zote za kisiasa, vinanyo fanywa na vyama vyote, sijaona familia au sehemu ya familia za viongozi hao wakiwa mstari wa mbele katika harakati za siasa, wengi wanaoumizwa katika vurugu hizo ni sisi akina kiherehere cha kutojua sheria za nchi na ushujaa wa kuwa tetea watu ambao kwa dhati kabisa hawatutambui, matokeo yake sisi tunafurahia kuwa daraja tu.

4. katika nchi ambazo tunaiga au ambazo demokrasia yake iko sawa, kila mwanasiasa lazima awe ni mwalimu wa uraia kwa wananchi wake, kwa maana kila atakachokuwa anasema lazima kiwe ni kumpa raia uwezo wa kuchanganua uwezo na sifa za mgombea. Leo Tanzania ni maajabu sana, siasa zetu ni mimi wa CHADEMA,CCM,CUF,UDP, n.k kwa lipi useme hilo! Kimsingi tungekuwa na uelewa wa juu kuhusu mambo ya urai, vyama vingebaki kuwa vyama -kwa maana ya Taasisi, pamoja na ukweli kuwa chama ni watu! Basi iwe ni watu ambao ni mkono(muhimili unaojitegemea)mwingine . Sisi wananchi tuwe pamoja, kila mgombea akija kutoka chama chochote tupime uwezo na sifa zake bila kujali mimi ni chama fulani. Tabia imejengwa mpaka mahali tunafika kusema leo mkutano ni wa chama fulani siendi kusikiliza..... kweli utapata viongozi sahihi kwa mfumo huuu! Acheni kulalamika kwa matunda ya viongozi wenu mliwachagua nyinyi wenyewe kwa nderemona vifijo.....

5. Wanasiasa kwa kufiiri sisi ni wajinga wameanza pia kutugombanisha na vyombo vya dola. Jambo hili ni ufinyu wa aidha mawazo ya wanasiasa wetu au ufinyu wa fikira na uelewa wetu kuhusu sheria na taratibu za nchi! Wao wabaki kama wao na sisi tubaki kama sisi! Tumeumiza sana, tumepoteza ndugu zetu kwa sababu tu maneno ya wanasiasa ambao hata familia zao huwa hawazipeleki.... Tumeshinikizwa kuvunja sheria za nchi kwa maslahi ya wanasiasa! Hakika kitakachotukomboa ni elimu ya ulaia. Kumbuka nilizaliwa huru, sina chama! Siwezi nikawa mtumwa wa chama hadi nipoteze maisha yangu... Niko huru kumchagua kiongozi yoyotekutoka chama chochote bila kujali ushabiki...

6. kumbuka ukiwa mshabiki hautapata kiongozi bora kutoka aidha ndani au nje ya chama chako! kwani hautapata muda wa kupima kauli na uwezo pamoja na sifa za viongozi wa vyama vya siasa! Haya shabikine mimi niko pembeni nawaangalia...! Kwani usipokushabikia hautapiga kura...? haya ndiyo mawazo yangu

7. Viongozi wanatafuta sifa kupitia matatizo/mateso ya wananchi kamwe hawafai!
 
japo imekuwa ndefu , lakini unatakiwa kufahamu kwamba ccm ndiyo wanaotufanya sisi wananchi wajinga , lakini tumeshtuka .
 
Kuna watu hawafanyi bidii kuboresha maisha yao, wanadhani kuna chama cha siasa kitakuja kuwaletea mkate na siagi mpaka mezani...
 
Khaa!!! umesema kweli lakini wakija washabiki watakupotezea. Tumekuwa ama tukiwachagua viongozi kwa kuangalia chain ya maslahi binafsi (mitandao) na siyo kwa uongozi bora kwa ajili ya nchi yetu. Tunamchagua mtu kwa kushawishiwa na jamaa/ndugu/rafiki zetu eti kwa sababu tukimchagua yeye atampa ulaji jamaa/ndugu/rafiki yetu nasi tutapata kuwa karibu na makombo ya keki ya Taifa huu ni ujinga. Kwa sababu wanadai kuwa wanataka tuwachague ili watutumikie basi tusikilize ahadi zao kisha watupe mpango wao wa utekelezaji kwa phases zinazowiana na muda. Kama muda fulani umefika na mpango haujatekelezwa kwa kipindi hicho basi kiongozi huyu lazima ajiuzulu. Huu uongo wa kudanganywa mara maisha bora kwa kila mtanzania mara mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000/ mara sijui nitawajaza mapesa mfukoni bila kutueleza utekelezaji utakuwa vipi ni kutufanya wajinga. Kama wakiendelea hivyo 2015 bora kuuza kadi ya kupigia kura ili anagalau upate nawe angalau kidogo :bored::bored:
 
Good understanding!
 
Back
Top Bottom