Siamini TBC1 kama ni Shirika la umma lenye Kutenda haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siamini TBC1 kama ni Shirika la umma lenye Kutenda haki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jnuswe, May 11, 2011.

 1. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Awali kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 nilikuwa nikiipenda sana TBC1 lakini tangu wafanye madudu yale katika utangazaji wa matokeo, sina hamu nayo, M. Hassan alipokuwa akitaja jina la mbuge wa cdm aliyeshinda katika jimbo mojawapo, aliwahi kutamka jimbo hilo limekwenda kwa cdm na akasema sijui huyu mbunge anaitwa nani, anaposema hayo alikuwa na jina mkononi la yule Mbunge na akalisoma kwa kujichanganya changanya,

  Leo kilichonudhi zaidi katika kipindi chao cha asubuhi wakati wa kupokea ujumbe mbalimbali kutoka kwa wasikilizaji

  Aliyekuwepo studio amekatisha kusoma ujumbe wa mtu, kwa kipande alichokisoma kilisomwa hivi "Serikali ni kweli imefilisika kwa maana hata wazabuni wana...." yule msomaji akakatisha kusoma ujumbe ule.

  Nimeumia sana ,uhuru wa mtu kutoa maoni uko wapi? nikawaza kuwa pengine huyu mtu aliyekatishiwa ujumbe wake ni Mzabuni na anauchungu wa kutokulipwa deni lake au alikuwa na hoja na mfano wa wazabuni wanayo idai serikali lakini ndo hivyo ujumbe wake ukakatishwa kusomwa
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya kuwataka TBC angalao wawe wakweli kwa kutupilia mbali hiyo kaulimbiu yao ya "uwazi na ukweli." Nasema hivyo kwasababu hivi karibuni nilimsikia mkugenzi wa redio hiyo mpya Bw. Mshana akitamka wazi kwamba kabla ya kutangaza jambo lolote redio hiyo kwanza inapashwa ipime hadhari yake kwa amani na umoja wa taifa. Ni dhahiri sera kama hiyo haiwezi kutoa fursa kwa wafanyakazi wake kufanya kazi yao kwa kujiamini; mara nyingi watakuwa wakiogopa ya kuwa wakitangaza habari kwa mfano za CDM ambayo imetangazwa na viongozi wa serikali kuwa inachochea vurugu uenda wakapoteza kitumbua chao, na hivyo katika kujihami mara nyingi wakati wa kufanya mahojiano na viongozi wa vyama vya siasa, utaona wanahojiana na Mbatia, Mrema au Cheyo wanaojulikana kuwa vibaraka wa chama tawala. Lakini mtu anajiuliza huyo Mbatia au Cheyo au Mrema ni wananchi wangapi wanaunga mkono chama chake hadi awe msemaji wao!
   
Loading...