PreGE2025 ‎Siaga Njega atia nia, ubunge jimbo la Mbagala

PreGE2025 ‎Siaga Njega atia nia, ubunge jimbo la Mbagala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za Ubunge limeanza rasmi ambapo leo June 28 watia nia kutoka sehemu mbali mbali katika Jiji la Dar es salaam wamejitokeza kuchukua fomu hizo.



Siaga Njega ni mmoja kati ya watia nia wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mbagala rasmi leo june 28 amechukua fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Temeke Jijini Dar es salaam.



Baada ya kuchukua fomu Njega amepata nafasi ya kuzungumza kwa uchache kile ambacho kimempelekea kuamua kujitosa kuwania nafasi hiyo licha ya jimbo la Mbagala kuwaniwa na vigogo wengi.


Amesema jimbo hilo limekuwa na wabunge wengi ambao ushirikiano wao na wananchi ni wachini sana hali ambayo inapelekea kuzorota kwa baadhi ya mambo ambayo yanawapa adha wananchi wa jimbo hilo.



Njega amegusia suala zima la ajira kwa vijana ambao wapo mtaani hawana ajira na kusema atafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanapata fursa mbali mbali zitakazo wasaidia kujikimu katika maisha yao ya kila siku.


Suala la bima kwa vijana waliojiajiri kwenye kazi za kusukuma matolori na mikokoteni amesema ni kazi ngumu lakini wanahitaji kuangaliwa kwa ukaribu ili angalau waweze kupatiwa bima zitakazo wasaidia kupata matibabu haraka wanapopata changamoto za kiafya.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025


Njega amekuwepo Mbagala kwa zaidi ya miaka 20 amesema changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo anazijua kwahiyo kilichobaki ni kupitishwa na baadae kwenda kwa wananchi kupata ridhaa.


Ikumbukwe jimbo la Mbagala sasa limegawanywa zamani lilikuwa linajumuishwa mpaka Chamazi, baada ya mgawanyo huo Chamazi nalo ni jimbo ambalo linajitegemea.

 
Back
Top Bottom