Si wote wanaopokea bahasha- Ngeleja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si wote wanaopokea bahasha- Ngeleja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,346
  Trophy Points: 280
  WAZIRI wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja amesema kuwa si viongozi wote wanaoingia katika Mgodi wa Buzwagi wanapewa bahasha za kaki na kushindwa kushughulikia mgogoro wa fidia za watu waliohamishwa kupisha uwekezaji huo.

  Waziri Ngeleja aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara baada ya wananchi kuonesha kutokuwa na imani na viongozi wanaokuja hapa kushugulikia mgogoro uliopo baina ya wananchi wa kijiji hicho kiliochopo kando ya Mgodi wa Buzwagi kuhusu mapunjo ya fidia.

  Katika mkutano huo uliofanyika kijiji jirani cha Mwendakulima, wananchi hao walisema kuwa kumekuwa na tabia ya viongozi kutoka serikalini kuja katika mgodi huo kwa madai kuwa wanashughulikia suala hilo na kuondoka, huku wakiacha matumaini yasiyofikiwa kwa wananchi kuwa suala lao la malipo litashughulikiwa.

  Walisema kuwa Agosti 2008, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Adamu Malima alifika katika kata hiyo kwa lengo la kusuluhisha mgogoro huo na kudai kuwa angerudi baada ya miezi mitatu, lakini ahadi hiyo haikukelezwa, hali ambayo imewapa wasiwasi wananchi wao.

  “Viongozi wengi wameshafika hapa na kungia katika mgodi huo na kukaa kabla ya kuzungumza na wananchi, jambo ambalo linatufanya tudhani kuwa hupewa bahasha za kaki (Fedha), jambo ambalo linatutia wasiwasi sisi,” alisema mmoja wa wananchi hao.

  Kutokana na madai hayo, Waziri Ngeleja alisema kuwa yeye hawezi kupewa bahasha hizo za kaki, na kusisitiza kuwa si viongozi wote wanapewa bahasha hizo.

  “Si viongozi wote wanaopewa bahasha hizo za kaki, kwani kuna viongozi wengine bahasha hizo hazingiliki kabisa," alisema na kuwataka wawe na imani na serikali yao inayofuatilia mgogoro huo," alisema.

  Wananchi waliohamishwa katika Kata ya Mwendakulima bado wanapingana na fidia zilizotolewa na mwekezaji wa Mgodi wa Buzwagi, kwa madai kuwa fidia iliyotolewa kwa kuhamishwa wananchi wa eneo hilo kuwa ndogo, jambo ambalo limezua mgogoro mkubwa baina yao na serikali.

  Katika hatua nyingine, Bw. Ngeleja alilazimika kuhutubia hadi usiku ili kutoa ufafanuzi wa kuchelewa kwa fidia hiyo na kuwapa wakati mgumu polisi waliokuwa wanalinda mkutano huo.

  Waziri Ngeleja alisema baada ya tume ndogo iliyokuwa imeundwa na serikali juu ya madai ya wananchi kuwasilisha taarifa, ilibainika kuwa madai yaliyokuwa ya msingi ni 194.

  Alisema kuwa mengi ya madai hayo yameshatatuliwa na kubaki 23, ambayo alisema angekutana na wahusika kuanzia jana katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

  Waziri Ngereja alisema serikali imepanga katika wiki hii itahakikisha ufumbuzi wa kero juu madai ya mali za wananchi yakiwemo ya fidia katika mgodi wa Buzwagi uliopo katika Kata ya Mwendakulim yanatatuliwa au kwisha kabisa.

  source: majira
   
 2. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ngeleja ni mchukuaji mzuri wa vibahasha, Ukweli huo anaujua vizuri Bwana Mihayo wa Buzwagi, Kuna wakati Mihayo nusura wanainchi wamtoe roho wakati Ngeleja keshaulaza Dar
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kama apokei bahasha amalize ilotatizo mara moja aache story
   
 4. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani akipokea atakili hadharani kuwa kapokea, Kama ajapokea kwanini ashindwe kushughulikia mamatizo wakati anamamlaka ya kushughulikia, aache upuuzi kwani amekuwa anatetea sana wawekezaji wezi wa madini bila sababu za msingi
   
 5. M

  Magehema JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda kaluli ya Mh. Ngeleja, si wote ila kauli yake inakiri kwamba wapo wanaopokea bahasha, kwanini hawatake actions kwa hao wachukua bahasha? Au na yeye anawapa muda wajirekebishe?
   
Loading...