Si sahihi kulinganisha ya Zimbabwe na Tanzania

Si sahihi kulinganisha ya Zimbabwe na Tanzania

Lekachonka

Member
Joined
Dec 17, 2016
Posts
35
Reaction score
17
Kila mtu amekuwa akitoa maoni yake kulingana na mtazamo wake kisiasa kuhusu Zimbabwe ya Mugabe na hapa kwetu Tanzania.

Kuna wanaohusisha moja kwa moja ZANU-PF na CCM na wapo pia wanaomlinganisha Rais Mugabe na Rais Magufuli,lakini pia wapo wanaolinganisha hayo mambo ya Rais Mugabe na mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Mbowe.

Ukisoma na kusikiliza hoja za pande zote,unaona zimejaa ushabiki tu wa kisiasa na hamna hoja ya maana waliyonayo. Hii inaonesha kwa kiasi gani tulivyo wavivu wa kusoma na kufuatilia kwa makini matukio makubwa yanayoendela duniani.

Ya Zimbabwe tuwaachie wazimbabwe, japo yametuachia cha kujifunza kama vyama,serikali na Taifa kwa ujumla.

Ukifuatilia watu makini,unamwona Rais Museveni tayari keshachukua hatua katika serikali yake kufuatia mkasa huu wa Zimbabwe. Na naamini vyama vingi hasa vikongwe Barani Afrika vitazidi kuchukua hatua sahihi kuhusu hili sakata.

AFRIKA NI MOJA,TUZIDI IOMBEA ZIMBABWE IPITE SALAMA KATIKA KIPINDI HIKI.
 
Mkuu Mi nilidhani unatoa sababu (facts) kwanini tusilinganishe Tanzania na Zimbabwe .
Kumbe umetoa maelezo ya katazo tu.

Uwe na Wiki njema na Asubuhi njema
 
Kwanza wanao mlinganisha one of the greatest orator afrika na Magufuli walifeli darasa la 7
 
Rais Mugabe ameondolewa madarakani kwasababu kubwa ni mke wake ambaye alitumia umri wa Rais Mugabe katika kutwaa madaraka. Hao wanaomfananisha Rais Magufuli na Mugabe wamefilisika ki sera na hawajui wanachokisema.
 
Rais Mugabe ameondolewa madarakani kwasababu kubwa ni mke wake ambaye alitumia umri wa Rais Mugabe katika kutwaa madaraka. Hao wanaomfananisha Rais Magufuli na Mugabe wamefilisika ki sera na hawajui wanachokisema.


..Zimbabwe jeshi lao limefungamana mno na chama tawala Zanu-PF.

..kwa maoni yangu Jeshi linataka kumpachika mwana Zanu-PF atakayemrithi Mzee Mugabe.

..nadhani SOMO lililopo mbele yetu wa Tz ni kuhakikisha kwamba tunaepuka kufunganisha vyombo vyetu vya dola na vyama vya siasa.

..Tukifanya makosa kama Zimbabwe basi kuna siku vyombo vya dola vitaingia michakato ya vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom