Si "date" na wanawake wachovu!

Una roho ngumu sana!
 
Kumbe wewe ni baharia(dume)? Bado hakuna maajabu, chuo ni miaka mitatu, ada kwa mwaka 1.5M, kwa miaka mitatu ni 4.5M, hiyo hela ya kawaida mno, hata mkuu wa shule anaweza kukulipia ada na mahitaji ya chakula na makazi.
 
Wanaume wenye hela mara nyingi wavivu kutype sasa ukiona vicomment uchwara ujue Ni miayo tu,,

Abarikiwe Sana huko aliko huyo mkaka unamsaidia mtu na hujionyeshi jamani, Kuna malaika wamo humu duniani
Huo ni mtazamo wako, mwanaume mwenye hela ana sh. ngapi ili ujue kuwa ana hela?
 
Nani kamdhalilisha mwanamke? Amejidhalilisha mwenyewe! Acha ugigisi!
 
Kumbe wewe ni baharia(dume)? Bado hakuna maajabu, chuo ni miaka mitatu, ada kwa mwaka 1.5M, kwa miaka mitatu ni 4.5M, hiyo hela ya kawaida mno, hata mkuu wa shule anaweza kukulipia ada na mahitaji ya chakula na makazi.
mimi ni baharia kumbe ulikua haujui.... dume la miraba minne, ni kweli ni ya kawaida kabisa hela ya chai na maandazi tu hiyo
 
Mimi sishangai kwa vile mahabaria wengi hiyo hali tumekutana nayo sana. Mwaka 2008 nilikuwa na denti mmoja tulikuwa kidato cha nne na nilimwelewa sana kuliko alivyojua na maisha yangu yalikuwa ya kimaskini japo hata yeye kwao hakuwa njema ila alinikataa na kukimbilia kwa vijana mboga 7, alinipa mawazo sana nikasema ipo siku mambo yanabadilika. Tulipomaliza kidato cha 4 tulipotezana maana alifeli akawa anarisiti kupata sifa za kuendelea na kidato cha tano nami 2009 nikaendalea na kidato cha tano na tulipotezana kabisa na hakuwa tena kichwani mwangu.

Mwaka 2021 mwezi 8 hivi akanipigia akanisalimia na kujitambulisha nami nikamwambia asante kwa kunikumbuka ila nipo busy nikakata simu. Jioni nikamcheki nikaongea nae akanambia yupo dar , nakauliza familia hsijambo akasema haijambo, nikauliza una watoto wangapi akasema 4 na mmoja yupo darasa la 5 nikasema hongera ila vipi mmeo hajambo akasema hana mme nikauliza hao watoto wa nani kama huna mme akajibu watoto hao 4 babazao tofauti nilicheka sana huku yeye akilia maana watoto wanasumbua njaa na hana hata sh ya chakula. Baadae kidogo akasema anaomba 3000 tu ili watoto wapate kula hakika huruma ilinipata moyoni nikasema pole alafu nikamtumia 20,000 alishukuru sana then nikamwambia kwa heri nipo kazini.

Wadada kuna umri huwa mnajisahau sana na kuwa na dharau mbaya na huwa hamjui kuwa mambo yanabadilika. Acheni dharau maana unayemdharau ipo siku utajua ndo msaada wako ila namna ya kumuanza utaona aibu.
 
KK kuwa Gentlemen mwanamke halingiwi ki umen ungemtoa na fifty ya ubber alafu ukamshit
Huwa napenda sana kufanya hivi

Yupo mmoja mara ya kwanza kaniambia nimkopeshe elfu 10 nikampa mara ya pili kaja kulialia nimkopeshe elf 20 nimempa halafu sina habari nae siku namsalimia anajifanya kuniuliza, "eti unanidai sh ngapi?" Mimi nikamjibu, "nimesahau"
Nikitaka kuondoka nikafanye shughuri zangu ananisemesha nikamuona miyeyusho tu, nikaachana nae
 
Vizuri, una haki ya kuishi upendavyo. Kila mtu anashinda mechi zake, mimi kwangu hapana aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…