Shyrose ashupalia adhabu ya Azzan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shyrose ashupalia adhabu ya Azzan

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 24, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi Wetu

  MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Shyrose Bhanji jana aligeuka mbogo kwenye kikao cha halmashauri hiyo kutokana na agenda iliyopenyezwa ya baadhi ya wajumbe kutaka mbunge wa Kinondoni, Bw. Iddi Azzan asamehewe adhabu kufuatia kauli yake ya hivi karibuni kudai wajumbe wa sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam ni mafisadi hivyo hawana budi kujiuzulu.

  Habari zinasema, wabunge wawili kutoka majimbo mawili ya mkoa wa Dar es Salaam ndio walikuwa mstari wa mbele kumtetea, Bw. Azzan pamoja na Katibu wa Wazee Mkoa, Bw. Mohammed Mtulya.

  Hata hivyo baada ya Mwenyekiti wa Wazee kuomba Bw. Azzan aombe radhi ili aweze kusamehewa, ndipo inadaiwa Bi. Shyrose alisimama na kupinga vikali hoja ya mwenyekiti na wajumbe wengine kwa kusema kuwa Bw. Azzan ni vema akathibitisha kauli yake vinginevyo aendelee kutumikia adhabu hiyo.

  Kikao hicho kilichofanyika juzi katika Manispaa ya Kinondoni kilikuwa maalumu kutathmini uchaguzi mkuu uliopita mwaka jana. Hata hivyo kikao kilitawaliwa na malumbano kati ya kundi la Bw. Azzan na kundi la Shyrose baada ya kundi la Azzan kudaiwa kutaka asemehewe adhabu hiyo.

  "Tuacheni kuwa wanafiki haiingii akilini kwa baadhi ya wajumbe wenye akili zao timamu kusimama na kuanza kumtetea Iddi Azzan...Iddi ametoa tuhuma nzito kwamba Sekretarieti ya Mkoa kuwa ni mafisadi sasa athibitishe kauli yake vinginevyo kwa kiongozi kama yeye kutoa maneno ambayo hayana ukweli ni sifa mbaya," mmoja wa wajumbe alimkakariri Shyrose akilalamika kwenye mkutano huo.

  Inadaiwa kwamba Bi Shyrose ambaye alishindwa kwenye kura za maoni jimbo la Kinondoni, alimtaka Katibu wa Wazee Mkoa wa Dar es Salaam kutoyumba katika kuitumikia nafasi hiyo vinginevyo atajishushia heshima kwa kuendekeza masuala ambayo hayana tija kwa chama.

  Malumbano kati ya kambi ya Bw. Azzan na Bi Shyrose yaliteka mkutano huo na kujikuta ukiacha ajenda ya msingi ya uchaguzi.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tatizo la Shyrose Bhanji ni kuwa yeye na Idd Azzam wote ni wanasiasa kutokana na Azimio La Zanzibar, bila hilo Azimio wasingekuwa madarakani na kujipenyeza kwa Maswali yao binafsi.

  Hawa ni watu wa kuwaogopa sana kwenye Siasa za Nchi Hii... Miaka ile Siasa ya watu wa form four unapata F na sasa hivi unagombea Ubunge?
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Bado sakata la CHATANDA arusha linafuka moshi.
  CCM naionea huruma.
   
 4. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  wacha wafu wazikwe na wafu wenzao,wacha wajimalize wenyewe
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Ni mwarabu mwenzake au??
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,401
  Likes Received: 3,727
  Trophy Points: 280
  Azzan nakushauri ...........USIJE UKADHANI CCM WANAMAANISHA WANCHOKISEMA...................... Angalia ulipofikishwa kwa kuunga mkonoi kauli zao....................

  HIVI UMESHAMSIKIA MUASISI WA KUJIVUA GAMBA KWA CCM AKITAJA HAO MAGAMBA NI AKINA NANI..........???? KUNA MWENYE UBAVU WA KUFANYA HIVYO ...............???? Na ndiyo maana hata hao wanaotajwa kuwa ni magamba wengine wamejibu kuwa WAO HAWAFAHAMU KAMA WAO NI MAGAMBA.
   
Loading...