Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,508
- 830,009
Papa ni aina ya samaki jamii ya kamongo... Wana harufu kali sana... Waliowahi kufika Tanga maeneo yale ya mabanda ya papa wanaweza kupata picha kamili... Ila kuna watu wamekulia pale kiasi kwamba harufu ile sio kikwazo kwao wameizoea.
Kimsingi hakuna Shurubati ya papa wala kamongo... Supu yake yenyewe ni shida... Utainywaje kwanza! Wakati kipande kidogo sana cha nyama yake kinakutosha kabisa kumaliza sima.
Kuna mamlaka nazichukulia kama Shurubati ya papa, Shurubati ya kamongo kutokana na matendo yao.. Tusaidie kuiponya nchi, tulisaidie TAIFA letu lisiangamie.. Lakini tunapotaka kulisaidia tuwe makini sana... Nilimsoma kwa majonzi kijana wa Arusha aliyeunguzwa makanyagio yake vibaya kabisa.
Sijamsahau pia wa chuo kikuu yule wa hostel... Kuna siku naye atasimulia kilichompata huko aliko na vile alivyotendewa... Hawa ni wachache kati ya wengi waliojaribu kuliponya taifa kwa kupaza sauti za wazi
Askofu Zakaria Kakobe imethibitishwa na mamlaka ya usalama wetu kuwa atahojiwa kutokana na matamshi yake ibadani.
Pengine anayefuatia ni Askofu Bagonza wa KKKT... Wote hawa walikuwa wanajaribu kuiponya nchi.
Wiki hii kuna uvumi ulienea mitandaoni kwamba mkuu wa nchi kapata tuzo ya amani kupitia mfuko wa Mandela ( JF imekuwa mhanga pia) shukrani wamekuwa wamekuwa waungwana na kuomba radhi huku mada husika ikipigwa kufuli
Nimeshangazwa na ukimya wa mamlaka na vitengo vyake... Hivi hawakulijua hili mapema? Kwanini wakaaa kimya? Hawakusoma? Kwanini waliacha uzushi usambae kwa karibia siku NNE nzima? Hii ni aibu Jamani ya akina Kakobe yamerukiwa haraka sana.
Hili la upotoshaji halijaonekana... Hakika mtu akinambia hakuna Shurubati ya papa wala kamongo nitambishia MILELE