Shule za kata zimekwenda na muasisi wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule za kata zimekwenda na muasisi wake?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Jan 19, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ukisoma katiba yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hakuna sehemu inayotamka rasmi kuwa kiongozi atayewajibishwa au kujiuzulu kwa manufaa ya umma anapoondoka kwenye madaraka ndani ya serikali ataondoka na mipango yote aliyokuwa akiisimamia.Pia hakuna ibara katika katiba hiyo hiyo inayokataza utekelezaji wa mambo yaliyokwisha achwa na aliyejiuzulu au kustaafishwa kwa manufaa ya umma.Inatia aibu katika nchi yetu kila lililoanzishwa na kiongozi ama akihamishwa wizara au kutenguliwa madaraka yaliyokuwa nayo na mikakati yake pia huondolewa ndani ya meza.Wote tumekuwa mashuhuda kwa hili ninalo lizungumza ndani ya thread hii.

  Shule za kata zilipoanzishwa ilikuwa ni kwa lengo zuri tu,lakini implementation yake na effort ili kuwa tofauti na maudhui ya mwasisi wake.Lengo lilikuwa ni kuleta elimu yenye tija katika kizazi hiki na kijacho.Haikuwa lengo kujenga majengo kwa nguvu za wananchi na kuishia hapo bila kuweka mahitaji halisi kwa watumiaji wa shule hizo.Haikuwa nia ya serikali inayoongozwa na mh. J Kikwete chini ya waziri mkuu aliyepima na kujiuzulu wadhifa wa uwaziri mkuu kwa shule hizo kukosa miundo mbinu ya elimu.Wazo lilikuwa zuri lakini mara baada ya mh huyo kuachia ngazi suala hili liliachwa na hakuna aliyelitilia mkazo.Utata huo umenisababisha kuandika thread hii ni kutokana na ukosefu wa umakini katika kusimamia dhana nzima na umuhimu wa elimu katika jamii.Shule hizi zimekuwa kiwanda cha kuzalisha daraja sifuri kutokana na mfumo duni.Sipendi kuamini waziri mkuu tuliye naye hakuliona hili wakati ni mkakati wa serikali hii iliyopo madarakani.Haiwezekani uwaziri mkuu ukawa ni mtu na si ofisi.Iko wapi mipango ya serikali ya muda mrefu,wa kati na mfupi,mbona kwa suala hili serikali inazidi kuprove failure!?Zamani mfumo wa elimu nchi mwetu ulileta ushindani katika jamii.Watoto waliofaulu ilikuwa ni shangwe kwenye familia husika pamoja na shule iliyomsababisha kufaulu,uko wapi motisha ule uliosababisha ushindani wa shule mmoja na nyigine?Haingii akili watoto wetu walioandaliwa kuingia katika shule hizi wanapimwa ufahamu wao kama wanajua kusoma na kuandika tu.Kama ni sera ya serikali elimu ya lazima ni kidato cha nne, itangaze rasmi.Wasiwasi wangu kwa staili hii tunakwenda kuwa wasindikizaji katika muundo wa jumuiya ya Afrika Mashariki.Nasema hivyo kutokana na miundo mbinu duni kwa shule hizi.Waalimu hakuna,madawati ni kama msamiati hazina maabara tunategemea elimu bora au bora elimu?Wizara imejaza madokta mbona hatuoni impact ya taaluma zao katika kusaidia kuboresha huduma za elimu.Leo kiwango cha forgery kwa watahiniwa kimeongezeka maradufu lakini hakuna hatua madhubuti kudhibiti hali hii.

  Tamati,nakaribisha michango yenu wana JF ilituweze kuboresha mfumo huu duni wa elimu,vinginevyo tunaandaa taifa la watu mbumbu na wauza vitumbua katika jamii zetu.Serikali iwe iongeze umakini katika kusimamia ilichokiamini kabla ya kuachana nacho na kurukia mipango mingine.Naomba kuwakilisha
   
Loading...