Sikubaliani na kufutwa kwa shule za binafsi hata kidogo, Serikali ijaribu kuwajali na kuwaheshimu Waalimu wa shule za Serikali, sio viongozi kuwagaia vimada wao fedha ya nchi na kuwaacha wawekezaji wafanye wanavyotaka na madini yetu, Serikali iwe makini katika ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali na kutumia kwa manufaa ya Wananchi wake na Taifa kwa ujumla sio kujijengea majumba kama mahekalu, wao, watoto wao na vimada wao, wawajali waalimu, madaktari na wafanyakazi wengine wa ofisi zao, unafikiri shule za binafsi zikifungwa mfumo mbovu katika elimu ndio utaisha kabisa, hao waalimu watakaotoka huko wanaweza kuamua kufanya shughuli nyingine, kama biashara, kufanya kazi kwenye mabenki au kwenda kufundisha kwenye shule nyingine nchi za jirani, na wazazi wenye uwezo kuwapeleka watoto wao wakasome nchi za jirani au Ulaya, cha msingi boresheni mazingira ya utoji elimu kwa ujumla na kuwajali Waalimu, ili wawe na moyo na ari ya kufundishwa kama taaluma yao inavyohitaji wafanye, msiwafanye wajute kuwa waalimu, waupuuze uwalimu na kufanya shughuli nyingine, hao wanaouza mitihani kwani hawajulikani miaka yote hii?!, wao na wizara yao wawajibishwe, kila mara wimbo ni huo huo, mbona hawatajwi ili wawajibishwe, wanaendelea kuachwa wakitajirika na biashara hii kwanini?!, who are they?!