kotinkarwak
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 376
- 115
Unashangaa zero na 4 kwa shule za watoto wenye vipaji maalum? hiyo ni kutokana na uchakachuaji ngazi walizotoka, siku hizi kuchakachua na kufaulisha sana ni sifa ya kumuongezea mtu idadi ya wanafunzi na hivyo mapato. Utashangaa mengi na huu utitiri wa shule binafsi za wafanyabiashara ambao hela ni kwanza mengine yote baadaye.
Zifutwe na serikali ipi? ya CCM?
Kaulize hizo shule zinazoitwa Saint ..... (yaani shule za watakatifu) zinamilikiwa na akina nani! Wabunge wa CC_, wakurugenzi wa serikali ya CC_, mawaziri wa serikali ya CC_, wenyeviti wa taasisi za CC_, wastaafu wa serikali ya CC_, n.k.
Haziko kwenye orodha ya kampuni za biashara na hawalipi kodi kwa vile ni shule za watakatifu ..... ingawa ada zake ni kuanzia 1m kwa mwaka na kuendelea hata kama ni za chekechea.
tukisema zifutwe kweli hatuta fika wanafunzi wengi siku iz itoshe shule za serekari zenyewe chach watafuta credeti watasoma wapi kama haito bado idadi ya watu inapanda kwa kasi tukizi funga tutasoma kweli. Ila nakubali ana na wewe kusema ni ghalama sana bac tuombe serekeri iweze kuzuia na kusimamia pia kubalansi ada zitozwazo na shule za watu binafsi kama ilivo kwa smatrd kwenye usafili!
The good thing kila mtu yuko huru kutoa maoni, bad thing mtu anasema chochote kile, mie nilifikiri serikali ipunguziwe mzigo wa kuendesha shule na secta nyingine wakati sekta binafsi imeonyesha inaweza kuleta mabadiliko makubwa mazuri na kwa kipindi kifupi kuliko serikali iliyokuwa hewani 5o+ years na bado wanapiga jaramba katika mipango mikakati, sera na ilani zao.
Sekta binafsi ipewe uwezo na kuamniwa zaidi sasa, performance ya shule binafsi ni nzuri na inataia moyo na hakuna mhitimu asiyejua kusoma wala kuandika. Changamoto zipo na lazima ziwepo ili vichwa vifanye kazi na hili pia linagusa na sekta binafsi
ni bora ziwe na ubia fulani na serikali na sio kuzifuta kwa serikali yetu haina uwezo kwa kila kitu kama huduma kwa jamii,wafanye kama hizi hospitali za taasisi binafsi na za dini ambazo ziko katika mpango wa DDH sijui,ili shule ziendelee na zikaguliwe ubora wa elimusio bora kufaulisha.utasikia matokeo kata ya kwanza,tarafa ya kwanza,kiwilya ya kwanza ya kimkoa ya pili ya kitaifa ya kwanza,mlete mwanao ada m3.pia wanapita kuchagua wanafunzi wenye uwezo kwenye shule za msingi na kuwachukua kesho yake eti wao wanatoa taaluma safi.tuwe macho.
Kwa kuzingatia hali ya mporomoko wa elimu, shule za watu binafsi zifutwe. Shule hizi zimechangia kuua elimu tena bila hata huruma, hawa jamaa wamegeuza elimu ya taifa hili kuwa ni biashara wakti serikali wakiangalia. Waziri wa elimu taifisha shule hizi kwa kuwapa fidia wamiliki.
Shule zibaki kuwa za mashirika ya dini, taasisi za umma na serikali tu.
Hebu fikiria wizi wa mithani ni hizi english medium, ada kubwa yaani wizi wa kuaminiwa, elimu duni yaani watoto hawafundishwi kama ambavyo inatengazwa na kuonekana kwa TV, Je mtoto atapata elimu kwa lugha asiyoijua?? as lower as class 1 or 2 at 7&8yrs of age????
Elimu biashara inamchango mkubwa kwenye kufa kwa elimu TZ, eti mtu anafaulu hajui kusoma wala kuandika haya ni mambo ya elimu biashara. WAZIRI FUTEENI SHULE ZA BINAFSI.
Nawasilisha
kazi kweli kweli. hivi huwa hampitii madaftari ya watoto wenu. Unaambiwa mtoto ni Bright, umewahi kummuliza swali na kupata ukweli. au unasubiri matokeo yaliyopikwa ya mwisho wa muhula, then ya taifa baada ya kuwafanyia mitihani?
Pole wee, utakuja kuumbuka asubuhi kumekucha, na baridi limeshakupiga usiku kucha.
Hapa kila mtu achukue hatua kivyake, hakuna aliyekushika mkono ukaibiwe na kudanganywa kwenye hizo shule.
chukua hatua.