fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,073
Kwa kuzingatia hali ya mporomoko wa elimu, shule za watu binafsi zifutwe. Shule hizi zimechangia kuua elimu tena bila hata huruma, hawa jamaa wamegeuza elimu ya taifa hili kuwa ni biashara wakti serikali wakiangalia. Waziri wa elimu taifisha shule hizi kwa kuwapa fidia wamiliki.
Shule zibaki kuwa za mashirika ya dini, taasisi za umma na serikali tu.
Hebu fikiria wizi wa mithani ni hizi english medium, ada kubwa yaani wizi wa kuaminiwa, elimu duni yaani watoto hawafundishwi kama ambavyo inatengazwa na kuonekana kwa TV, Je mtoto atapata elimu kwa lugha asiyoijua?? as lower as class 1 or 2 at 7&8yrs of age????
Elimu biashara inamchango mkubwa kwenye kufa kwa elimu TZ, eti mtu anafaulu hajui kusoma wala kuandika haya ni mambo ya elimu biashara. WAZIRI FUTEENI SHULE ZA BINAFSI.
Nawasilisha
Kwa kuzingatia hali ya mporomoko wa elimu, shule za watu binafsi zifutwe. Shule hizi zimechangia kuua elimu tena bila hata huruma, hawa jamaa wamegeuza elimu ya taifa hili kuwa ni biashara wakti serikali wakiangalia. Waziri wa elimu taifisha shule hizi kwa kuwapa fidia wamiliki.
Shule zibaki kuwa za mashirika ya dini, taasisi za umma na serikali tu.
Hebu fikiria wizi wa mithani ni hizi english medium, ada kubwa yaani wizi wa kuaminiwa, elimu duni yaani watoto hawafundishwi kama ambavyo inatengazwa na kuonekana kwa TV, Je mtoto atapata elimu kwa lugha asiyoijua?? as lower as class 1 or 2 at 7&8yrs of age????
Elimu biashara inamchango mkubwa kwenye kufa kwa elimu TZ, eti mtu anafaulu hajui kusoma wala kuandika haya ni mambo ya elimu biashara. WAZIRI FUTEENI SHULE ZA BINAFSI.
Nawasilisha
Kama jina lako lilivyo mkuu nadhani "ungefikiri" kabla ya kupost hapa jamvini.
Jaribu kufafanua shule binafsi zinaua vipi elimu na wakati inabidi zifaulishe ili kujitangaza kwa wananchi?
Wazo la kutaifisha umelifikiria vyema? Huoni kama hili ni gumu kutekelezeka kwa kuwa hizo tu shule chache ambazo serikali ina dhamana nazo inashindwa kuzihudumia ipasavyo!
Hapa kwenye "...eti mtu anafaulu hajui kusoma wala kuandika..." nimeshindwa kukuelewa maana mitihani yote ya taifa inahusisha kuandika na ili uandike inabidi usome maswali, sasa kweli hata kama kuna uizi wa hiyo mitihani unataka kusema watu huingia na papers ambazo wameshajibiwa! mmh hii sidhani kama inaingia akilini.
Mkuu mi nadhani ungetoa wazo la serikali kuwa na mamlaka kwa ajili ya kusimamia huduma ya elimu ya msingi na sekondari, kama ilivyo kwa Trca katika mawasiliano au Ewura katika nishati au TCU na NACTE kwa vyuo.
Hakuna usimamizi yakinifu, zaidi serikali imeweka nguvu kubwa kwenye usimamizi wa mitihani tu kupitia NECTA na kusahau kuwa mitihani ni hitimisho tu la kile mwanafunzi alichoambulia akiwa shuleni.
ngoja nipite maana ukichangia naweza kujikuta namtukana mleta mada nikaishia kupigwa ban, kwaheri fikirikwanza
Zifutwe na serikali ipi? ya CCM?
Kaulize hizo shule zinazoitwa Saint ..... (yaani shule za watakatifu) zinamilikiwa na akina nani! Wabunge wa CC_, wakurugenzi wa serikali ya CC_, mawaziri wa serikali ya CC_, wenyeviti wa taasisi za CC_, wastaafu wa serikali ya CC_, n.k.
Haziko kwenye orodha ya kampuni za biashara na hawalipi kodi kwa vile ni shule za watakatifu ..... ingawa ada zake ni kuanzia 1m kwa mwaka na kuendelea hata kama ni za chekechea.
HII NDO inatutafuna, wakubwa ndo wamiliki wa hizi shule-ZINAUA JAMII KIELIMU harafu hakuna la kufanya. Kama kiingereza ni elimu basi ziendelee; lakni ukweli ni JANGA mtoto anajifunza kwa lugha ngeni eti atakuwa thinker au claimer wa mambo tangu mtoto tunaviona zinakariri, leo hatuoni madhara ya hili; nchi zote zilizoendelea zinafundisha kwa lugha ya mama walau kwetu kiswahili nyerere alikifikisha pazuri tungetumia hadi University.
Lipo la kufanya.
Kwanza tusipinge kama kiswahili au kiingereza ndio kitumike kutoa mafunzo, nyuzi nyingi hapa zimesha'discuss hilo swali au tatizo lenyewe ni ACCESS ya hiyo elimu. Bila kutoa judgement kuwa private schools wanatoa elimu nzuri au kuwa wanaiba mitihani na kuwa na pass rate kubwa, inabidi tu ujiulize kweli elimu pale inapatikana? Nadhani utagundua kuwa nyenzo za kutimiza ahadi ya elimu wanayo, walimu, vitendea kazi n.k.
Lakufanya ni lipi? Hatutoendeleza elimu bila sisi wakereketwa kuwa mstari wa mbele kuishinikiza serikali kufanya kweli kwenye sekta hii, lakini pia, wazazi na walezi inabidi watoe mchango wao katika kuendeleza elimu. Tukumbuke, kuwa sio pesa peke yake itatatua tatizo lenyewe, wazazi/walezi inabidi kujua na kufuatilia kwa umakini elimu watoto wao wanayopata na hapo labda patakuwa na mabadiliko. Tisulalamike tu wakati matokeo yanatangazwa kuwa failure rate imepanda, lakini kila siku tujiulize, hawa watoto wanapotoka kwenda shule, je wanaambulia nini?!
Je elimu ni biashara? Ndio, na maudhui ya biashara sio tu kupata faida, kama mzazi unampeleka mwanao shule X kwani inatumia ST Fulani bila kujua kwa undani kama kweli mwanao atapata elimu, wewe ndio wakulaumiwa, wewe ndie unaharibu hiyo biashara na kuwafanya wamiliki wasiwe na changamoto kuendeleza elimu bali tu kukupa a pass rate ya uongo na kweli, Wazazi wakifuatilia na kujua nini kinacho fundishwa na value yake, basi elimu itolewe na serikali au watu binafsi hapo elimu itakuwa na manufaa.
Mabadiliko ya kweli hayaletwi kwa njia ya mapinduzi,suala hapa ni kuboresha mazingira ya hii sekta muhimu!Una uhakika gani kama shule za serikali zinaweza kuchukua wanafunzi wa nchi nzima!?
Zifutwe?? Labda hizo shule hazimilikiwi na watunga sheria!!