Shule za Academia hizo!!

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,469
281
nimeiona ktk blogu flani hapa...kazi ipo

Mkuu wa kazi Michuzi.
Nakusabahi..
Kwa heshima na taadhima naomba unifikishie ujumbe huu kwa wadau. Hili jambo sio mara ya kwanza kutokea na kuripotiwa na kama inavyoonyesha hapa, wahusika hawapendi mambo haya yafike kwenye vyombo vya dola na vya habari. Wanapenda kuyamaliza kimya kimya ili shule zao zisiathirike ki-hadhi (reputation) na kibiashara!!!.


Hawajali na kulinda haki na utu wa watoto kwa nguvu na gharama zozote hata ikibidi kuathirika nilikokusema. Tumwamini nani? Usalama wa watoto wetu uko wapi? Ni nini kifanyike kuzuia haya mambo? Sio watoto wote watakuwa na ujasiri wa kusema.


Sio wazazi wote wenye umakini wa kuwachunguza watoto wao wanapotoka mashuleni, wengi hurudi nyumbani usiku wanakuta watoto wameshalala na watoto asubuhi huandaliwa mapema sana na haraka haraka sana kuwahi school bus (lazima wazazi tuwajibike, hakuna excuse). Tusipopata jawabu la ulinzi mashuleni na ndani ya mabasi watoto wetu kutoka kwa mamlaka za shule, watapona kweli?

Mdau Anon.....
Asante.

hoja.jpg
 
Back
Top Bottom