Shule yenye darasa la re-sitters kwa ajili ya form four | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule yenye darasa la re-sitters kwa ajili ya form four

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Tosha, Feb 15, 2012.

 1. Tosha

  Tosha Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Wanajamvini naomba ushauri juu ya shule nzuri ya bweni ambayo inapokea na ina darasa la wanafunzi wanaorudia mitihani ya kidato cha nne kama watahiniwa wa kujitegemea(Private Candidate) au re-sitters!

  Najua Jitegemee Secondary walikuwa na darasa kam hilo japo wao ni day halikadhalika Makongo Secondary,hata hivyo nimeangalia kwenye matokeo ya form four lakini sijaona matokeo yao ya Private Candidates katika shule hizi!

  Naomba ushauri kama unaijua shule yenye walimu na mazingira mazuri ambayo ina darasa la re-sitters na kama ina kituo cha kufanyia mitihani na mwisho ikiwa ni ya bweni ni nzuri zaidi! Tafadhari naomba ushauri juu ya jambo hili!
   
 2. S

  Sharp Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Na kwa upande wa mikoani ni wapi naweza kupata shule za kuresit form four au kumpokea kwa ajili ya A level mwanafunzi mwenye div IV ambaye combination inakubali masomo mawili KL kwa pass za DC? Msaada tafadhali.
   
 3. +255

  +255 JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Morogoro kuna shule inaitwa Alfagem wanatoa hy service. Jaribu kuangalia kwanza matokeo yao ya PC ka utalidhishwa nayo.
   
 4. S

  Sharp Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Asante kaka, ngoja niwatafute.
   
 5. Tosha

  Tosha Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  asante sana kwa kunijuza inaonekana "soko" la darasa la re-sitters lipo kubwa lakini shule bado ni chache sana anyway inabidi kukubalinana na hali halisi!asante kwa ushauri
   
 6. m

  mahmoud abbas Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kijana nenda hapo jitegemee kapige skul kwan now days wanayo mabweni kwa wanaorudia mitihani ila kaza buti broda...
   
 7. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  MOROGORO kuna shule inaitwa Alfgerm aka kwa pekupeku, boarding ni wasichana tu, iko makini ingawa majengo yake hayavutii. kuna masister wa kikatoliki inASEMEKANA wanaawaamsha wanafunzi saa 8 USIKU kukamua. pekupeku MWENYEWE ana wabana maticha wanafundisha si mchezo. Ila kama mwanao ni mayai usipeleke lazima akusumbue, mANAKE shule hiyo ni full discipline. Ila akibahatika kumaliza shule, hata kama hatafaulu anatoka amejifunza maisha hakusumbui tena. Pia Kusoma bible knowledge ni lazima, kama hutaki unasepa.
   
 8. N

  Njangula Senior Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuelekeza Itamba ss -ipo wilaya Makete- Iringa kiutawala lakini kimahusiano ipo Mbeya zaidi. Hudtma safi ni ya kanisa KKKT. Ni boarding reassiters na school candidates.so text HM 0753744136
   
 9. dottoz

  dottoz JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 805
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 80
  Piga chuo 2 broda mambo ya kurudia yalishapita na wakati kama vp pga msuli.
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Usiwe na mawazo mgando kama shibuda na mwigulu, koz kinachomata ni uwezo 2 basi, kama dogo ana uwezo na anajiamini mwache arudie na atatoka 2, pia kama we ulishindwa jua akili hazifanani.
   
 11. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hivi ada yao pale bweni inaweza kuwa kiasi gani? Kuna dogo wangu ningependa aende pale ila mi niko mkoani. Mwenye kujua msaada tafadhali.
   
 12. Tosha

  Tosha Member

  #12
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  1. Ada inatofautiana baina ya mwanafunzi mmoja na mwingine
  2.Atayechukua masomo mengi atalipia kiasi kikubwa
  3. mwanafunzi aliyepata credit mmoja tu atapaswa kurudia masomo manne au zaidi, wa credit mbili atapaswa kurudia msomo matatu au zidi na ambaye hana kabisa credit atapaswa kurudia masomo matano au ziadi aliyepata divison O atalazimika kuridia masomo saba au zaidi.
  4.Somo moja kwa mwezi ni TShs 8000 so unapiga hesabu idadi ya masomo then unazidisha na miezi ya kusoma wastani ni kama 7 au 8 hivi
  Gharama nyinginezo;
  1.wanaosoma masomo ya sayansi watalipia Tshs 20,000 kwa kila somo moja kwa ajili ya madawa kwenye laboratory
  2. Mchango wa maendeleo ya maktaba tshs 25,000
  3.tests tshs 20,000
  4.malipo ya kituo km mtu atafanyia hap Mgulani JKT
  5.kwa watakaopenda kufanya real practical NECTA watalipia 20,000 kwa kila somo moja la sayansi
  6. Fomu italipiwa Tshs 10,000
  7. Gharama ya sare(shati,surauli/sketi,viatu,tai,socks,nembo na tshirts) ni 60,000
  Kiasi chote cha fedha kinalipwa kwa MKUPUO MMOJA

  Kila mwanafunzi atalazimika kushughulikia UANDIKISHAJI kwa ajili ya mtihani wa taifa YEYE MWENYEWE na kila atakaye fuata mpango huu wa re-sitters atalazimika KUTII sheria na kanuni zote za JITEGEMEE(JKT) shule ya sekondari

  Maelezo yote hayo nimeyatoa katika fomu yao ya kujiunga na kikundi cha kurudia mithani ya kidato cha IV. Uniwie radhi katika fomu hakuna maelezo juu ya BWENI japo najua wana HOSTELI natumaini watakuja wengine kukujuza
   
 13. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Shukrani mkuu. Gharama za hostel hazijahusishwa au sijaelewa vizuri?
   
 14. Matti

  Matti Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kuna KIMASEKI SECONDARY SCHOOL , Arusha. ina hostel kwa wasichana tuu.
  Kuna MAJENGO HIGH SCHOOL , Moshi. ina hostel.
  Kuna Enaboishu high schoo l, Arusha, boarding.
  Kuna Arusha Meru Secondary school, arusha, ni day.
   
Loading...