Shule yageuzwa kituo cha ngono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule yageuzwa kituo cha ngono

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Oct 22, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KUKOSEKANA kwa uzio katika Shule ya Msingi Nyahanga, wilayani Kahama, kumewapa mwanya wahuni kutumia madarasa ya shule hiyo kama sehemu ya kuvutia bangi na kufanyia mapenzi baada majira ya usiku.
  Hayo yalibainishwa juzi na walimu wa shule hiyo mbele ya waandishi wa habari waliotembelea shuleni hapo kubaini changamoto zinazowakabili.
  Walisema kuwa genge la wahuni hao limeligeuza eneo hilo kama kituo chao cha starehe na hivyo kufanya litakavyo wakati wa usiku.
  Walimu hao walisema kuwa hali hiyo inatokana na miundombinu ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1942 kuwa mibovu, kiasi cha kuwafanya wanafunzi waliosoma hapo miaka ya nyuma, kuchangishana ili kuinusuru.
  Walibainisha kuwa shule hiyo haina vyoo vya kutosha, nyumba za walimu, vitabu vya kufundishia hasa kwa wanafunzi wa darasa la nne ambao hukaa zaidi ya 80 katika darasa badala ya 45 kama ilivyo ada.
  Mkuu wa shule hiyo, Lucas Matanyanga, alisema kuwa tayari amekwishatoa taarifa katika kituo cha polisi cha wilaya ili kuwadhibiti wavuta bangi hao na watu wanaotumia madarasa kufanyia ngono.
   
Loading...