Shule ya sekondari Mingumbi haina choo, wanafunzi wanajisaidia porini.

emkey

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
728
136
Habari wakuu,
Naandika mada hii nikiwa na masikitiko tele. Ni kuwa, shule tajwa hapo juu ambayo inamilikiwa na serikali, ipo wilayani Kilwa, Mkoani Lindi. Shule hii ya Mingumbi sekondari ina wanafunzi kadhaa wa jinsia tofauti lakini haina vyoo vya wanafunzi na walimu pia, na ikitokea mwanafunzi kabanwa na haja aidha kubwa au ndogo, mwanafunzi anaenda maporini kwa ajili kujisaidia.
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa iliwahi kutoa fedha za ujenzi na kumpatia Mtendaji wa Kata ya Mingumbi aitwaye Rashidi Issa, naye amekula hela hizo na kila siku anadai ataleta mafundi wa kutengeneza choo lakini hamna kinachoendelea. Suala hili la choo limewahi kufika hadi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa lakini hakuna hatua anazochukuliwa.
Kwa Rais wetu JPM na wasaidizi wake ni wachapakazi, naomba mulifanyie kazi suala hili kwa mustakabali wa elimu na watoto wetu.

Nawasilisha,
Mzazi.
 
Acha warutubishe mimea porini..maisha kutegemeana,misitu inatutegema na sisi tun aitegea pia.
 
KWELI KAZI IPO RAIS AFUATILIE UJENZI WA CHOO?
KAMATI YA MAENDELEO YA KIJIJI AU KATA ipo likizo? Kwanini msihamasishane kuchangia fedha na nguvu kazi? KACHUKUENI MFANO MOSHI, WANAJITOLEA Michango wanajenga ndo serikali imatoa pesa ya kumalizia

"KIDUMU CHAMA CHA KIPINDUPINDU"
 
Mie Nikadhani Mwigumbi Pale Jirani Na Mgodi Wa Almas Mwadui,kumbe Huko?Wanye Tu Maporini,yataoza Tu.
 
Back
Top Bottom