Shule ya Sekondari Kiboriloni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule ya Sekondari Kiboriloni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nick, Feb 28, 2011.

 1. N

  Nick Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Jambo la kushangaza na aibu kubwa kwa shule ya sekondari Kiboriloni kwa yale yaliyowatokea wiki iliyopita. Kumejitokeza kundi la madent (ke) kuhudhuria nyumba za wageni (guest house) hapo hapo Kiborilini na kusingizizia wapo shule. Huamka na kujianda kwa shule ila hawaendi shuleni. Walipogundulika shuleni, waalim walilazimika kuwatia mboko hadi za ziada. Nasema za ziada kwani baada ya kichapo tuu wasichana hao watano wa shule hiyo walitoroka kabisa nyumbani na shuleni kisa kilichowalazimu wazazi wao kulala nje (Holili na kituo cha polisi Majengo) kwa siku mbili. Iligundulika kuna mtandao wa watu huwa wanawarubuni wasichana wadogo kuwapatia kazi Kenya. Hivyo huwatorosha bila ya ridhaa ya wazazi, kuwapeleka Kenya kwa kazi za ndani au danguro. hii iligundulika mara ya kumbana aliyetajwa na mmoja wao aliyeachwa njiani (Himo) baada ya kugundilika kwamba eti ni mja mzito. kijana aliyetajwa alipatiwa kibano cha polisi ambapo alilazimika kuwasiliana na mtandao wao ili wawaachi madenti hao. Hivyo wasichana hao wanne wakapatikana Tarakia Rombo mpakani na Kenya siku ya tatu bila ya wao kula cho chote. Walibanwa (madenti) polisi Majengo na kukiri yote haya ni ya kweli na kumtambua kijana aliyetajwa na mwenzao, wakaandika maelezo na kuruhusiwa kwenda na wazazi wao nyumbani ili warudi leo J3. Kijana aliyetajwa huko magereza hadi leo.
  Tuwaombe kwa Mungu msamaha na wimbi hili ya kutoroshwa kwa wasichana haswa manispaa ya Moshi kwani ilitokea soko la mbuyuni na inasemekana tena Korongoni.
  Mungu ibariki Tanzania
   
Loading...