Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,699
- 119,333
Imethibitishwa kuwa wanawake wakijengewa uwezo wa kujiamini, wanauwezo wa kushinda katika chaguzi mbalimbali bila kuhitajika hitaji la upendeleo wa kutengewa viti maalum, kwa sababu wanawake wana uwezo sawa na wanaume na hata kuwazidi wanaume kwenye kila kitu, ikiwemo kwenye siasa na kwenye uongozi.
Uthibitisho huo, umethibitishwa katika uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mt. Kibo iliyopo Mbezi Juu jijini Dar es Salaam, ambayo ni shule mchanyiko wa wavulana na wasichana, lakini katika uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi wa shule hiyo, uliofanyika mwishoni mwa wiki, nafasi zote za uongozi wa juu, zimeshikwa na wanafunzi wa kike waliochaguliwa kidemokrasia baada ya kuwabwaga wapinzani wao ambao ni wanafunzi wa kiume.
Ushindi huo umewezekana baada ya uongozi wa shule hiyo, kuamua kufundisha somo la demokrasia kwa vitendo, katika azma ya shule hiyo kutekeleza hoja ya “samaki mkunje angali mbichi” kwa kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo, somo la demokrasia ya uchaguzi kwa vitendo, ili kupanda mbegu ya demokrasia kwa wanafunzi wa shule hiyo tangu wangali wadogo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sebastian Ngimba, amesema, lengo la mafunzo hayo ya demokrasia kwa vitendo, ni kuwafunza wanafunzi hao jinsi demokrasia inavyofanya kazi, tangu wakiwa wadogo, ili watakapo kuwa watu wazima na kuingia kwenye siasa, wawe wamepata msingi imara wa demokrasia tangu wangali wadogo.
Mafunzo hayo yamefanywa kupitia uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi kupangwa kufanyika kidemokrrasia kwa kufuata taratibu kama za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, ambapo iliundwa kamati ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wa uchaguzi, wagombea wote wakajaza fomu za kugombea, wakapitishwa, wakapiga kampeni za wazi, kisha uchaguzi ukafanyika kwa karatasi za kura zilizochapwa majina ya wagombea na kupigwa kwa kura za siri kupitia masanduku ya kura yanaoonyesha (transparent), kura zikahesabiwa, na matokeo yakatangazwa na washindi kuapishwa kushika uongozi.
Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa shule hiyo Aristides Peter Mugisha amesema wameendesha uchaguzi wa viongozi wa shule yao kwa kufuata taratibu kama za NEC katika kuendesha uchaguzi ambao umefuata kanuni za uchaguzi huru na wa haki. Makamo Mwenyekiti wa kamati hiyo Arieth Albert amesema wameendesha uchaguzi huo kidemokasia hivyo walioshinda, wameshinda kwa haki na kihalali.
Katika uchaguzi huo, nafasi zote tatu za juu za viongozi wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo, zimeshikwa na wagombea wasichana ambao wamewashinda wavulana, katika hali inayoonyesha, watoto wa kike, wakijengewa uwezo wa kujiamini tangu wakiwa shuleni, wanauwezo wa kushindana na wanaume na kushinda, katika hali itakoyopelekea siku zijazo, kutohitajika tena kwa wanawake kutengewa nafasi za upendeleo wa viti maalu, kwa sababu, uchaguzi wao umethibitisha wanawake wanaweza, na wanauwezo sawa na wanaume na wakati mwingine, wanawake wana uwezo wa juu zaidi hata kuwashinda wanaume.
Viongozi hao wapya ambao ni Dada Mkuu Nancy Mary Mtinga, na Dada Mkuu Msaidizi Magreth Musagusa na Mkuu wa nidhamu, Angel Jacob, wamesema wameweza kuwashinda wanaume kwa sababu, shule yao ya Mt. Kibo, wamefunzwa kujiamini kuwa wanawake wanaweza, na wamegombea na wanafunzi wa kiume, wamepiga kampeni na wamewashinda vibaya wagombea wa kiume.
Mwalimu Prosper Shimili amesema wanafunzi wa kike sio tuu wanauwezo wa kushinda chaguzi, hata darasani, kuna wanafunzi wengi wa kike wanauwezo mkubwa kimasomo kuliko wanaume, hivyo wanafanya vizuri kuliko wanafunzi wa kiume.
Mwalimu Doreen Msangi, amesema ili juhudi hizi za kuwajengea wanawake uwezo wa kujiamini zizae matunda, ni lazima juhudi hizo ziazie nyumbani katika level ya familia, kwa wazazi, familia na jamii, ziwape fursa sawa watoto wa kike na wa kiume, sio kuwaambia kazi fulani ni za kike na nyingine ni za kiume.
Sensa ya watu na makazi imethibitisha idadi ya wanawake ni wengi kuliko wanaume, hivyo kama wapigakura wanawake tuu wangewachagua wagombea wanawake, hakuna wagombea wanaume wangeshinda chaguzi.
NB. Habari hii pia ilitangazwa, kwenye Redio, kwenye TV, kwenye magazeti, kwenye Blogs na You Tube.
9:02
MT. KIBO PRIMARY SCHOOL YAFUNDISHA DEMOKRASIA KWA VITENDO.
-
Shule ya MT. Kibo Primary School Yafundisha Demokrasia kwa Vitendo-TV News on Channel Ten.
Blog: MATUKIO @ MICHUZI BLOG
Post: Wanawake, wanauwezo wa kushinda chaguzi kuliko wanaume, hivyo hawahitaji viti maalum
Link: MATUKIO @ MICHUZI BLOG: Wanawake, wanauwezo wa kushinda chaguzi kuliko wanaume, hivyo hawahitaji viti maalum
-