Habari za kutwa Wazee wa jukwaa. Ninaomba kwa anaye faham shule nzuri ya kiislam kwa mtoto wa kike. Mwanangu anategemea kuanza darasa la kwanza mwakani panapo majaaliwa.
Nimefikiria swala la kumpeleka boarding school kwa shule za Kiislam ili akapate elim dunia na akhera. Napendelea sana eneo la DSM kwani ni rahisi hata kumjulia hali kwa karibuni mara kwa mara.
Mambo ya kuzingatia:
1. Maadili mazuri
2. Ufauru mzuri
3. Mazingira mazuri yenye usalama na malez mazuri
4. Gharama nafuu
Mkuu kwa umri huo nakushauri usimpeleke shule yeyote ya kiislamu wala ya kikristo.
Kwa umri huo anahitaji zaidi malezi ya wazazi,ungalizi wao na mapenzi yao.
Wasio na wazazi wanatamani wangekuwa na wazazi wao kila siku.
Wasio na watoto wanatamani wangekuwa na watoto wao kila siku.
Wenye watoto wanataka kupeleka watoto wao boding skuli.
Mkuu wanawake wa zamani wasomi hawakuwa wanaitafuta elimu kwa mfumo wa kukaa boding na walikuwa wanaelimika vizuri tu.
Kwangu mimi boding ina hasara kuliko faida,mwache nyumbani mumfundishe tabia njema na huku akirudi shule aende zake madrasa hata kama kwa wiki siku mbili ndo anasoma huyo,hana cha kuharakia katika elimu ya dini,mtume alitumia miaka zaidi ya ishirini kufundisha uislamu.
Kumbuka kuwa ukikaa na mtoto nyumbani unamfunza na tabia na adabu njema,ukimpeleka hukoboding sasa anaweza kujifunza dini na dunia lakini tabia ikawa anajifunza kwa wenzie,hivyo tabia ikawa mbovu.
Unaweza kusema kuwa "si atajifunza tabia kwenye dini akishasoma" hili jambo usilitegemee sana kwa sababu kuna tofauti ya dini na tabia.
Ili ufuate mafundisho ya dini basi mara nyingi unatakiwa uwe na tabia njema uliyofundushwa na walezi wako wa karibu.
Kaa na mwanao mfundishe tabia njema aende shule arudi aende madrasa atakuwa salama zaidi kuliko huko boarding