Kuna shule nyingine naijua. Ina majengo mazuri sana ya MMEM (wahusika hawakuiba huko) na ina watoto 500. Ila ina waalimu watatu tu (Mwalimu mkuu, mke wake na mwlimu mwingine mmoja). Darasa la kwanza hadi la saba. Kuna shule hapo? Let's be serious.
Ukiuliza serikali wanakwambia budget haitoshi. Kaangalie luxuries za masafari yasiyoisha na misafara ya rais. Ukifanya project moja ndogo tu, ukapunguza magari matatu katika msafara wa rais. Ukapunguza safari za rais nje ya nchi kwa nusu. Ukaondoa malipo ya per-diem kwa maofisa wa serikali wanaosafiri huku wamelipiwa full board (badala yake ukawalipa 20% incidental allowance); shule hizo itakuwa historia katika kipindi cha miaka mitano tuu.
Tunaomba kwa sababu tuna-mentality za kimaskini. We have all the money arround, ila haziendi huko zinapotakiwa kwenda. Hatuhitaji hata kuomba.
Kuna kodi nyingi mno kwa watanzania wa kawaida wanaopigania shilingi. Hizo hela zinakwenda wapi? We need a second independence!!