Shule kongwe ya Itete taabani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule kongwe ya Itete taabani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by HUNIJUI, Oct 20, 2012.

 1. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  WANAFUNZI wanaosoma katika shule kongwe ya Msingi Itete, mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoani Rukwa, wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo wazazi wao kudaiwa kugoma kuchangia madawati, hivyo kusababisha wengi wao kusoma wakiwa wameketi sakafuni katika darasani yao. Shule hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na Kanisa Katoliki ilianzishwa mwaka 1888 ambayo sasa ina zaidi ya wanafunzi 800, lakini majengo yake yakiwa yamechakaa huku sakafu za madarasa zikiwa na `mahandaki’ yaliyojaa vumbi, hali iliyoelezwa na baadhi ya wanafunzi kuwa si mazingira rafiki na hatari kwa afya zao.

  Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, umebaini kuwa wazazi wengi wamegoma kuchangia mahitaji muhimu kwa watoto wao wanaosoma shuleni hapo ikiwemo madawati na chakula kwa madai kuwa ni wajibu wa Serikali kutekeleza hayo ‘mgomo’ ambao baadhi ya viongozi wanadai unachochewa na wanasiasa ili watoto hao waichukie Serikali yao. Mwandishi wa habari hizi alishuhudia kila darasa lilikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosomea humo huku nusu yao wakiwa wameketi chini hali ambayo wengi wao wanadai inawawia vigumu kuwa wasikivu darasani.

  Lakini pia ilibainika kuwa wanafunzi katika shule hiyo iliyoanzishwa miaka 124 iliyopita, licha ya kutumikishwa na walimu kazi zikiwemo za kukusanya kuni na kuchota maji muda wa masomo, lakini wengi wao wanatembea pekupeku kwa madai kuwa wazazi wao hawana fedha za kuwanunulia viatu hata baadaye sare. Aidha, kutokana na uchakavu wa vyumba vya madarasa yanayofurika idadi kubwa ya wanafunzi walimu hulazimika kufundisha na kusahihisha madaftari ya wanafunzi wao wakiwa chini ya vivuli vya miti huku wanafunzi wakilazimika kupanga misusuru mrefu kusubiri zamu zao. Baadhi ya walimu shuleni hapo walipohojiwa na gazeti hili walikiri kuwa wanafunzi hulazimika kushinda na njaa shuleni hapo kutwa nzima kutokana na wazazi wao kutokuwa tayari kuchangia gharama za chakula pia wanalundikana na kukaa chini sakafuni madarasani, hali ambayo inazorotesha maendeleo yao.

  Hata kwa upande wa chakula cha mchana pia wazazi wamegoma kuchangia wakidai kuwa ni wajibu wa Serikali si wao hivyo kusababisha watoto wao kushinda na njaa kutwa nzima shuleni hapo,“ alisema mmoja wa walimu wa shule hiyo, Didas Katabi. Gazeti hili likiwa katika maeneo karibu na shule hiyo lilishuhudia baadhi ya wanafunzi wa kiume wakiwa wamebeba kuni na walipohojiwa kwa masharti ya majina yao kutoaandikwa gazetini walikiri kuwa hutumikishwa mara kadhaa na walimu wao kufanya kazi hizo zikiwemo kukusanya kuni na kuchota maji muda wa masomo
   
Loading...