Shule kinara kidato cha 6 taabani

Shule kinara kidato cha 6 taabani

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,367
Reaction score
27,773
SHULE ya Igowole, iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu, inakabiliwa na matatizo mengi, ikiwemo ukosefu wa mabweni, kiasi cha Mkuu wa Shule kulazimika kuhama nyuma kuachia wanafunzi wapate pa kulala.

Mbali na ukosefu wa mabweni ya kuhimili idadi ya wanafunzi, matatizo mengine ya shule hiyo ni ukosefu wa maji, maktaba, vifaa vya kufundishia na kusomea, gari la shule na walimu hasa wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Mkuu wa shule hiyo ya serikali iliyoko katika Kijiji cha Igowole wilayani Mufindi, Andrew Kauta, ameachia nyumba kwa ajili ya sehemu ya wanafunzi wa kike 237 wanaojiunga na kidato cha tano shuleni hapo.

Hata hivyo, shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1988 na kidato cha tano na sita kuanza mwaka 2008, pamoja na matatizo hayo, imeongoza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu, yaliyotangazwa hivi karibuni.

Kati ya wanafunzi 30 waliohitimu Kidato cha Sita mwaka jana, 19 walipata daraja la kwanza, 10 daraja la pili na mmoja ndiye mwenye daraja la tatu.

Kitendo cha kuibuka na matokeo mazuri, licha ya kuwepo changamoto hizo, kimekuna wadau wengi akiwemo Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola ambaye amesema mafanikio ya shule hiyo yanaonesha jinsi walimu na wanafunzi wake wasivyokatishwa tamaa.

Alisisitiza upo umuhimu mkubwa wa kupewa misaada wanayohitaji ili wafanye vizuri zaidi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkuu wa Shule alisema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, haijawahi kupokea wanafunzi wengi wa Kidato cha Tano kama ilivyotokea mwaka huu.

"Tangu elimu ya kidato cha tano na sita ianze kutolewa shuleni hapa mwaka 2008, tumekuwa tukipokea wastani wa wanafunzi 30 wa kidato cha tano kila mwaka," alisema Mkuu huyo.

Alisema mwaka huu, shule hiyo imeletewa wanafunzi wa kike 237 wa Kidato cha Tano, watakaoungana na 30 walioingia kidato cha sita. Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 900 kidato cha kwanza hadi cha sita.

Hata hivyo, mkuu huyo alisema shule ina bweni moja pekee lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wasiozidi 86. Alisema bweni hilo lililojengwa tangu shule ilipoanzishwa, miaka 26 iliyopita, haliko katika hali nzuri.

Alisema wanafunzi takribani 30 wa Kidato cha Tano, watajibana katika nyumba hiyo huku wengine 36 wakipelekwa katika bweni hilo pekee. Wanaobaki watahifadhiwa katika madarasa matatu, yanayotumiwa na wanafunzi wa vidato vya chini.

Mwalimu wa Taaluma, Isiaka Chodota alisema kutokana na sehemu ya madarasa kutumika kama mabweni, shule inabakiwa na vyumba 19 vya madarasa.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu na Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola waliahidi kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo ya shule hiyo, waliyoieleza kwamba mafanikio yake yameutoa kimasomaso mkoa wa Iringa.

Akizungumzia siri ya mafanikio ya shule hiyo katika matokeo ya Kidato cha Sita, Mkuu wa Shule alisema mwaka 2010 walijiwekea mpango mahususi wa miaka mitano wa kuboresha elimu katika shule hiyo, ikiwa ni pamoja na kusisitiza matumizi ya Kiingereza.

Siri nyingine ya mafanikio ya shule hiyo ni kuipa kipaumbele nidhamu. Kwa mujibu wa mkuu wa shule, kila Ijumaa huhakikisha wanafunzi na walimu wanakumbushwa sheria, kanuni na miiko ya shule.

Chanzo: Habarileo
 
Hii ndo bongo xaxa shule miaka yote unachukuaga wastani Wa wanafinzi 30 Tu,mwaka huu mnapeleka 237 huku hamjaboresha chochote mnategemea nn? Walimu hawatoshi,madarasa ndo hivyo tena,du kweli hiyo ndo #BRN
 
haya ndo mambo ya kishenzi, shule inauwezo wa kupokea wanafunzi 30, hao 207 wa ziada wanini?
 
Yaan kutoka wanafunzi 30 hadi 237 kuna watu nahisi wana funza vichwan au ndo mpango wa kutaka ididimie ili shule zao ziendelee kupeta
 
Mazingira ya shule hudetermine ufaulu.Hebu tuambi mwaka jana walifauluje? Tuone kama sio Kawambwa kabadilisha wanaofaulu kuwa wa mwisho and vise versa.
 
Mazingira ya shule hudetermine ufaulu.Hebu tuambi mwaka jana walifauluje? Tuone kama sio Kawambwa kabadilisha wanaofaulu kuwa wa mwisho and vise versa.

Hata mimi siamini haya matokeo mi naamin yamepikwa ili kuikweza BRN na maandalizi ya kampeni za mwaka kesho!
 
Huo utitiri wa wanafunzi sikilizia matokeo yao mwakani utachoka
Yaani waongeza wanafunzi wakati miundo mbinu iko pale pale si kukomoana uko?
 
Mnacho lalamikia nini? Mnajua kabisa bado hatuaminiani sisi wenye ngozi nyeusi,hasa sisi wa Tz! Leo tunaona nivema kumlundikia wanafunzi mwalimu wa Igowole ili mwaka ujao aonekane alibahatisha badala ya kumpa Moyo! Tulio wapa mamlaka ya kuendesha hizo shule(TAMISEMI/ WIZARA YA ELIMU) wanajua kabisa kuwa miundo mbinu ya shule ile imezidiwa,wanaongeza wanafunzi kwa idadi hiyo iliyo tajwa,bila kuboresha kituchochote! Ahh,labda wenzangu mnieleweshe huo ni WIVU,GERE,KIJICHO AU UHASIDI kwa Mwalim MKUU?
 
Mtiririko wa ufaulu kwa ile shule kwa miaka mitatu iliyopita siyo mbaya,ila mabweni hakuna yanatumika madarasa mawili hivi,
jiko ni dogo pia,na madarasa ya advance yapo mawili,
serikali inachanganya mambo hapa hawajatafakari kwa umakini.
 
Yaan kutoka wanafunzi 30 hadi 237 kuna watu nahisi wana funza vichwan au ndo mpango wa kutaka ididimie ili shule zao ziendelee kupeta

Hizo ni mbinu za uponyaji kwa ndugu yao, Mkuu wa shule ya Tambaza!Mimi sijui kapewa hiyo shule lini.Lakini kwa uzoefu wa serikali yetu ukifuatilia utakuta ni ndugu yake MZITO fulani aliyekuwa amepangiwa KINTIKU shule ya sekondari.Apate uzoefu huko ili siku zijazo apewe shule kubwa kama Tambaza! Lakini kwa sababu ni ndugu na MZITO fulani au alikuwa na uwezo wa kuhonga,basi matokeo ndiyo hayo! Kifuatacho ni kudhoofisha ufanisi wa M/mkuu wa Igowole hii ndiyo Tz!!!
 
Kwa ile shule binafsi ninaamini matokeo hayajapikwa,ni jitihada za mkuu wa shule pamoja na wanafunzi wenyewe,ila hili la kuongeza wanafunzi wengi hivyo something is wrong somewhere.
Hata mimi siamini haya matokeo mi naamin yamepikwa ili kuikweza BRN na maandalizi ya kampeni za mwaka kesho!
 
Tambaza fanyeni tour ya kitaaruma Igowole Sec School, maana mmejisahau
 
Mazingira ya shule hudetermine ufaulu.Hebu tuambi mwaka jana walifauluje? Tuone kama sio Kawambwa kabadilisha wanaofaulu kuwa wa mwisho and vise versa.


unataka kusema kati ya waliofaulu kwa alama za juu tunaweza kupekua na kuopoa mmoja wao hajui hata kuandika jina la shule yake? :thinking:
 
Back
Top Bottom