Shule ina mwalimu mmoja na wanafunzi 195, akisafiri inafungwa

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,536
Hivi Viwanda bila Wataalamu vitakuwaje au ndo tunatengeneza cheap labour? Nini maana ya kuwa na uongozi katika ngazi za chini kama wanashindwa kudeal na vitu kama hivi?

Mambo ya nchi hii yanaweza kukufanya uwe na hasira bila kupenda.

========

JANUARI 9, 2017 wanafunzi 195 wa Shule ya Msingi Matarawe katika Kijiji cha Marungu, Tarafa ya Mpepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, walikuwa wakiendelea na likizo licha ya kwamba ndiyo siku shule nyingi zilifunguliwa.

Siyo kwamba walitega shule, la hasha! Bali mwalimu pekee aliyepo, Gaudence Msuha, alikuwa amesafiri kwenda mjini Songea kuhudhuria mafunzo ya siku nane ya kujengewa uwezo masomo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) yaliyotolewa kwa walimu wote wa awali kutoka wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma kati ya Januari 10 hadi 18, 2017.

Hii haikuwa mara ya kwanza kufungwa kwa muda kwa shule hiyo yenye darasa la awali, la kwanza na la pili tangu ilipoanzishwa mwaka 2016.

Shule ina mwalimu mmoja na wanafunzi 195, akisafiri inafungwa | FikraPevu
 
Nilidhani nchi ina walimu wa kutosha.
hahaha umenifanya nicheke, ina walimu? we acha tu si tunaofanyaga kazi zetu vijijini ndo tunajua uozo wa serikali, na hiyo shule sijui kama watoto hawakai chini. ngoja baba yuko bize na kujenga chato iwe kama dubai harafu ndo atawarudia
 
Hivi Viwanda bila Wataalamu vitakuwaje au ndo tunatengeneza cheap labour? Nini maana ya kuwa na uongozi katika ngazi za chini kama wanashindwa kudeal na vitu kama hivi?

Mambo ya nchi hii yanaweza kukufanya uwe na hasira bila kupenda.

========

JANUARI 9, 2017 wanafunzi 195 wa Shule ya Msingi Matarawe katika Kijiji cha Marungu, Tarafa ya Mpepo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, walikuwa wakiendelea na likizo licha ya kwamba ndiyo siku shule nyingi zilifunguliwa.

Siyo kwamba walitega shule, la hasha! Bali mwalimu pekee aliyepo, Gaudence Msuha, alikuwa amesafiri kwenda mjini Songea kuhudhuria mafunzo ya siku nane ya kujengewa uwezo masomo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) yaliyotolewa kwa walimu wote wa awali kutoka wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma kati ya Januari 10 hadi 18, 2017.

Hii haikuwa mara ya kwanza kufungwa kwa muda kwa shule hiyo yenye darasa la awali, la kwanza na la pili tangu ilipoanzishwa mwaka 2016.

Shule ina mwalimu mmoja na wanafunzi 195, akisafiri inafungwa | FikraPevu
Hahaaaa mwenezenu kimwili nipo Tanzania kiakili marekani hata sijui kwanini.
 
Back
Top Bottom