Shule Dar yatoza ada ya shilingi 60 milioni!

Duhh!! Nimekosea njia.
Magufuli kusanya kodi kila senti inayolipwa
 
Hujaona jina la Magufuli, kiongozi wa serikali ni nani?

Unagahamu maana ya msemo wa "the buck stops with the president"?

Nani kakataa serikali kulinda raia wake?

Nani kakataa ada kuwa proportional na elimu inayotolewa?

Kama kuna watu wanataka elimu kama ya Groton Prep School bongo, na wana hela ya kulipia hivyo, kwa nini serikali iwapangie watu wa sekta binafsi ada?

Kwa nini serikali iingilie sekta binafsi? Hususan kama serikali hata haijaweza kuweka sawa shule zake yenyewe?

Serikali ijikite katika kuboresha shule zake, iachane na habari za kuoanga ada kwa shule binafsi.

Ama sivyo, itakuja kushindwa kuendesha shule zake na kuharibu za binafsi.
 
Kuna watu wanalipa ada ,siye wengine tunasindikiza ,ila sipo sure kama elimu inayotolewa hapo ni msaada kwa mtoto au ni kuharibiana maadili
 
Kwani kuna mtu ana tatizo hapo?! Manake haya mambo tutaanza kuhoji hadi bei za taasisi kama Hyatt Regency-The Kilimanjaro!!
 

Mkuu nadhani Prof.Joyce anaweza kumshauri Raisi vilivyo! Nategemea Uprof-wake hautabakia kama wa yule mama wa aliyekuwa ardhi!
Wizara yake ibakie kwenye kusimamia Kanuni na kwamba iwe na Wakaguzi makini wa kuzikagua shule hizi kuwa zinazingatia mitaala husika lakini kwa vyovyote Mitaala yao lazima iwe na maeneo yanayoihusu Nchi yetu Tanzania-iliko toka kihistoria kwenye maeneo ya Siasa,Uchumi na Kiutamaduni. Kwa Mfano tu Kwamba Sharti shule husika iwe inafundisha Kiswahili na Mwalimu Mtanzania aliyebobea kwenye Kiswahili.

Yako mengi ila Wizara iachane na eneo la Bei elekezi kwenye Biashara za Watu na Makampuni maana tumekubali Soko huru hivyo waache ijiendeshe!
 
Na hilo ndio jambo la muhimu zamani sisi tulikuwa tunaona aibu kusoma private school lakini sasa imekuwa kinyume chake!
 
Duh! Mimi kuanzia vidudu hadi la 12 sidhani kama milioni moja iliisha.
 
Kwani shule ipo hiyo tu. Sio lazima kumpeleka mwanao kusoma huko. huna uwezo peleka mwanao akasome bure. Hii serikali sijui ipoje. Wameacha kutumia muda wao kuboresha haya mashule yao, wapo tu hawajielewi
 
Ukiwa na hela nyingi hazina kazi ni vizuri kumpa mwanao elimu bora
Mkuu MKWEPA KODI,ni kuwa ukiwa na hela nyingi hata kama zina kazi,jambo la kwanza na la msingi ni kuhakikisha unampa mwanao elimu iliyo bora. Vile vile mkuu,ukiwa na hela chache/kidogo,hata kama hazikidhi mahitaji,ni vyema sana ukajitahidi pia kumpatia mtoto elimu iliyo bora.
 
Kwa hilo mimi sina tatizo ili mtadi kuna shule hadi za mlala hoi,mtu unajikuna unakopafikia
 
H
Kuna watu wanalipa ada ,siye wengine tunasindikiza ,ila sipo sure kama elimu inayotolewa hapo ni msaada kwa mtoto au ni kuharibiana maadili

Siumeambiwa kuna shule ktk izo,,watoto wanafuga dredi,wanakula ndumu,,na mixer kuvaa vihereni kwa wanafunzi wale masera,,,,,,
 
Hivi unalipa m30 alafu mtoto anafeli.... si kutafutiana lawama huku!!!
Mkuu tufanye mapato yako ya mwaka baada ya kodi na expenses zote ni million 500, kwanini mtoto asisome hiyo shule?
 
Mkuu au na kwenye hizi ada za private schools tuongezee na ka kodi flani ka 5% katika ada zinazolipwa ku support shule za serikali?ili kusaidia kuongeza ubora katika shule zetu za kata

Au kila mzazi wa mwanafunzi anayesoma tz achangie 5% ya ada + michango yote kusaidia shule zetu za za kata
 
umenena vema, na ninadhani wazazi huwapeleka watoto kwa ridhaa yao wenyewe bila kulazimishwa, kila mtu anampeleka mtoto shule inayolingana na uwezo wake, hata mimi ningekua nazo mwanangu angesoma hukohuko na watoto wa mabalozi

hii serikali ijifikirie mara mbili kabla ya kuamua maamuzi yake ya kijinga
 
hata kama zinatumia mitaala ya hapa bado hakuna ulazima wa kuwa na ada elekezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…