Shukrani

Shukrani

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
5,289
Reaction score
3,125
Habari za kazi Wana JF wenzangu,

Nilifiwa na Mama yangu mzazi tarehe 26/06/2011 na mazishi kufanyika tarehe 29/06/2011, niliondoka kwenda nyumbani (mkoani) tarehe 27/06/2011 kuwahi mazishi bila kutoa taarifa hapa JF. Hatahivyo, nachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wana JF, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliokuwa pamoja nami kwa hali na mali wakati wa kipindi kigumu na kuniwezesha kuwahi mazishi. Tulimaliza matanga tarehe o4/07/2011 na nimerudi eneo langu la kazi.
 
Habari za kazi Wana JF wenzangu,

Nilifiwa na Mama yangu mzazi tarehe 26/07/2011 na mazishi kufanyika tarehe 29/07/2011, niliondoka kwenda nyumbani (mkoani) tarehe 27/07/2011 kuwahi mazishi bila kutoa taarifa hapa JF. Hatahivyo, nachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wana JF, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliokuwa pamoja nami kwa hali na mali wakati wa kipindi kigumu na kuniwezesha kuwahi mazishi. Tulimaliza matanga tarehe o4/07/2011 na nimerudi eneo langu la kazi.

Hapo kwenye red sijaelewa vizuri???? Anyway pole sana Mungu awafariji nyote mlio na ukiwa wa kuachwa na ndugu zenu!
 
mkuu hizo tarehe mbona hazijafika?



Pole sana ndugu, Mungu awape wafiwa wote moyo wa subira katika wakati huu mgumu.

Hapo kwenye red nadhani ameghafilika tu @ bennynho
 
Oh, sorry tarehe ni za mwezi Juni.
 
Hapo kwenye red sijaelewa vizuri???? Anyway pole sana Mungu awafariji nyote mlio na ukiwa wa kuachwa na ndugu zenu!

Oh, sorry, tarehe ni 26/06/2011; 26/06/2011; 29/06/2011. Asante, lakini hiyo lugha uliyotumia "nyote mlio na ukiwa wa kuachwa na ndugu zenu", sio nzuri kwa sababu kwa kuwa nawe unaishi, ipo siku utakuwa miongoni mwetu wenye ukiwa.
 
Pole sana, Mungu ailaze roho ya Marehemu pema peponi!
 
Pole mkuu Sawabho-hao wana JF wengine walipata wapi habari hizo?Tuko wote kumuombea mom!
 
Pole sana Ndugu yangu

The JF family is with you my bro.
 
Back
Top Bottom