Shujaa Magufuli alikuwa ni jeshi la mtu mmoja aliyetegemea silaha ya kuteua na kutumbua, Bashiru usiamini kama kuna Sukuma Gang

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,023
Kiukweli hii kitu inaitwa Sukuma Gang haikuwa kitu halisi kwa sababu Shujaa Magufuli alikuwa ni Jeshi la Mtu mmoja aliyekamata mihimili yote mitatu.

Magufuli hakuwa na Wapambe ila Watu walijipendekeza Kwake ili wateuliwe na wengine walijipendekeza ili wasitumbuliwe.

Shujaa Magufuli aliweza kuwatumbua Rafiki zake wa karibu kabisa akina Kitwanga, Kichere, Kipilimba nk ndio Kusema yule Mwamba hakuamini Katika "Sisi" bali aliamini Katika "Mimi" kama ilivyo kwenye Biblia.

Nimshauri tu Dr Bashiru afanye kama anaomba radhi ili yaishe kwa sababu CCM siyo kama CUF ambayo maalim Seif alikuwa na Watu ambao leo Zitto Kabwe akipata msukosuko watamtetea kwa Nguvu zote kwa niaba ya Maalim Seif.

Mungu ni mwema Wakati wote!
 
Tuujue umri wako kwanza, Tanzania itaendelea ikipata rais ambae kwa Sasa amezaliwa 95 kwenda juu
The rest endeleeni kuchangamsha genge eti aombe msamaha oooh awe mnyenyekevu ooh kampa ubunge hivyo anyenyekee.

Hamuoni kuwa tunahitaji kuzungunza ukweli na huo ndio uzalendo? It's shame kuanzisha mada ya kishambenga kama hii
 
Bashiru ni kama kazungumza mawazo ya wengi.

Wapo watu wengi tu wanaokubaliana na kauli yake.

Hata naye akinyamaza au kunyamazishwa atakuja mwingine.

Kila kitu kina mwisho wake.

Hii tabia ya kukwapua mali za uma na kugeuza serikali kama mali ya watu wachache ina mwisho wake.

Yana mwisho haya.
 
Bashiru ni kama kazungumza mawazo ya wengi.

Wapo watu wengi tu wanaokubaliana na kauli yake.

Hata naye akinyamaza au kunyamazishwa atakuja mwingine.

Kila kitu kina mwisho wake.

Hii tabia ya kukwapua mali za uma na kugeuza serikali kama mali ya watu wachache ina mwisho wake.

Yana mwisho haya.
Hakunaga mawazo ya wengi Bongo Kila mtu anakufa na lake.
 
Kikweli kila uzi nakuta bashiru kasema hivi ila kiukweli sijajua kasema nini hadi kawa maarufu hivi?
 
Back
Top Bottom