Shujaa anapolalamika vitani baada ya kujipigapiga kifuani kwa majigambo

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Sasa hivi upinzani (I mean CDM na ACT) wanadai wamefanyiwa mchezo mbaya na chama tawala. Mwanzo walidai kuwa wagombea wao wananyimwa form. Hata kabla hawajatuambia tatizo la kunyimwa form limeishaje wamezuka na hoja mpya kuwa wanarudisha form lakini wanakuta watendaji hawapo maofisini. Ukiwa kichwa kimejaa hewa utaamini! Lakini tulia jiulize hivi: hivi wanarudisha form gani? Ambazo walinyimwa? Utarudishaje form ambayo ulidai hukupewa? Hivi tuamini lipi ndio limetokea? Kunyimwa kuchukua au kurudisha form?

Inabidi uwe na hewa ya hydrogen kichwani ndio utaamini komedi hii!

Ukweli ni kuwa wahusika walishapima upepo wakaona hauko sawa. Mkakati wao toka Alfa ulikuwa kuvuruga uchaguzi. Wamekuta mpinzani wao anazijua karata vyema. Hata sasa kuna uwezekano mkubwa watatekekeza phase III ya mpango wao: WATASUSA!

Nikumbushe?

Kabla zoezi la kuchukua form kuanza na mara tu lilipoanza kiongozi mkuu wa CHADEMA na ACT walitoa matamko. Kila mmoja kwa wakati wake alikinasibu kuwa hawawezi kumuachia nyani shamba! Wakaenda mbali zaidi na kudai ikiwa TAMISEMI itacheza mchezo mbaya wanaionya serekali kuwa itakutana na walichoita "nguvu ya umma" ngazi za mitaa.
Kauki hizi ziliashiria wamejiandaa vya kutosha iwe mvua iwe jua!

Sasa jua limewaka! Badala ya serikali kukutana na hiyo nguvu ya umma ni wao ndio wamekimbiwa na nguvu ya umma. Nguvu ya umma haina habari na malalamiko yao. Inasubiri siku ya kupiga kura ifike ifanye kazi yake ya msingi. Kuchagua viongozi wawatakao.

Mtu ungedhani baada ya kukosa kuungwa mkono na nguvu ya umma wataalam hawa wa kufungua kesi Kisutu mawazo wangeelekeza huko! Hawa ni wataalam wa kufungua hadi kesi za kupinga uteuzi unaofanywa na mkuu wa nchi. Nini sasa kinawazuia kuupeleka huo ushahidi walioukusanya mahakamani ili mahakama iamue ni kweli au si kweli? Wanalalamika ti kama kawaida yao au kweli wameonewa? Si wanadai Wana mawakili wasomi na wasioshindwa kesi? Waende mahakamani na ushahidi wa kunyimwa form au form kutopokelewa au hujuma nyingine yoyote. Sio kutuambia tu eti nchi inakoelekea ni kubaya!

Ni hivi: inategemea ulikoekeleza ubongo sio ulipoelekeza macho!

Tafsiri nyepesi ni kuwa hiyo nguvu ya umma iliyokataa kufuata amri yenu yenyewe inaona nchi inaelekea ilipotakiwa ielekee.

Nyie jidanganyeni kuwa inaelekea kubaya. Ndiko mlikoelekeza ubongo. Ukielekeza ubongo makaburini lazima uone kifo mbele yako!

Badala ya kutuambia mtandaoni kuna watu wamenyimwa au kukimbiwa pelekeni huo ushahidi mahakamani. Au mnaoamini kuwa tuhuma NI kweli wekeni huo ushahidi humu! Majina ya wahusika na maeneo husika. Ila msisahau kuupeleka na Kisutu.

Sisi hatuna hydrogen kwenye ubongo. Nyie ndio mnapinga hata ujenzi wa reli, ununuzi wa ndege, kuzuia makanikia, ujenzi wa bandari, n.k. Sasa leo mkituambia mmekimbiwa tuwaamini bila ushahidi? Nani aamini watu sampuli hii? Hata benki ukienda kuomba kazi unaulizwa umewahi kufungwa, kushitakiwa au kutuhumiwa kwa wizi? Ukijibu "ndiyo lakini mara moja tu" utaagwa! Huaminiki!

Subirini siku ifike mtaiona. Nyie bakini na ngonjera za kunyimwa na kukimbiwa!

Nguvu ya umma inasubiri kupiga kura!

Nilishawaasa kuwa tafuteni political retreat mjipange upya! Msipokiri kwamba watanzania wengi wamempata raisi waliyekuwa wakimuomba Mungu awapatie mtapata tabu sana!

JPM kakonga nyoyo za watanzania wengi mno. Kaeni chini mjiulize ni kwa nini?

Mkiendelea kujidanganya mna nguvu ya umma au eti watanzania wengi wanamchukia JPM OLE WENU!

ANAPENDWA MNOO NA WANYONGE WENGI

Mkiendelea kujidanganya mtafanya achukiwe kwa tweets na kupinga OLE WENU.

ANAYOFANYA YAMENUFAISHA WENGI
 
Back
Top Bottom