EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,086
Shujaa hafi, daima huendelea kuishi ndani ya mioyo ya watu kwa kupitia yale mema aliyoyafanya enzi za uhai wake. Ile alama aliyoiacha, namna alivyoyagusa maisha na mioyo ya wengi, kwa kadri alivyouishi uhalisia wake na kuisimamia nafasi yake kikamilifu enzi za uhai wake, hayo ndiyo humfanya mtu aonekane ni shujaa pale anapokuwa ameumaliza mwendo wake wa kuendelea kuishi hapa duniani.
Moyo ulipata ganzi ghafla, miguu ikakosa nguvu ya kuendelea kusimama, huku macho yakiukosa uvumilivu wa kuendelea kuyazuia machozi. Kwa kweli taarifa za kuondokewa na mpendwa wetu, rais wetu, ndugu yetu na mwafrika wa kweli Dkt. J. P. Magufuli, nilizipokea kwa mshituko na masikitiko makubwa sana kama ilivyokuwa kwa watanzania wengine. Hapo ndipo nilipoelewa, kumbe machozi huziwakilisha zile hisia nzito ambazo haziwezi kuonekana au kuelezeka hata kidogo kwa kupitia maneno au matendo yetu.
Nikiwa katika tafakuri na kuangalia mafunzo mhimu ninayoweza kuyapata kutokana na maisha ya mzee wetu Magufuli. Nimejikuta katika maswali haya: "ellyskywilly" tayari mzee wetu ameukamilisha mwendo wake. Enzi za uhai wake aliielewa vyema nafasi yake na akaisimamia kikamilifu kiasi ambacho alikuwa tayari kujitoa kama sadaka kwa ajili ya nafasi hiyo. Wewe nafasi yako ni ipi katika Dunia hii? Ni kwa kiwango gani unaisimamia nafasi hiyo? Maisha yako yana maana gani ikiwa hautaielewa nafasi yako katika duniani hii na kuamua kujitoa kama sadaka kwa ajili ya kuisimamia nafasi hiyo?
Maswali hayo yameongezea uchungu zaidi ndani yangu. Yameongeza kilio moyoni mwangu. Maswali hayo yamenifanya niendelee kuyachimba zaidi maisha yangu na kuangalia umhimu sasa wa kuyafanyia mabadiliko makubwa yenye tija.
Kwako rafiki unayeusoma ujumbe huu! Nafahamu fika kuwa, moyoni mwako kumejaa huzuni nzito kufuatia kifo cha mpendwa wetu. Hapa natamani nawe uingie kwenye tafakuri kama ilivyo kuwa kwangu, uangalie yale mafunzo unayoweza kuyapata kutokana na maisha ya aliyekuwa rais wetu. Usiishie kuumia na kuhuzunika moyoni, bali uhakikishe unaondoka na funzo kubwa la kukusaidia ili uweze kuyaishi maisha yenye tija.
Je, unaielewa vyema nafasi yako ndani ya Dunia hii?
Unataka Dunia ikukumbuke kwa lipi?
Upo tayari kujitoa kama sadaka kwa ajili ya kuisimamia nafasi hiyo?
Ni vyema tufahamu kwamba, Dunia itatukumbuka na kutuenzi kwakuwa tulizielewa vyema nafasi zetu na kuamua kuzisimamia nafasi hizo kwa uaminifu mkubwa. Dunia haitatukumbuka kwa sababu ya magari na majumba ya kifahari tuliyokuwa nayo wala kwa idadi ya starehe tulizozifanya. Dunia itatukumbuka kutokana na juhudi kubwa tuliyokuwa nayo katika kuhakikisha tunazisimamia nafasi tulizokuwa nazo na kuyagusa maisha ya walio wengi kwa kupitia nafasi hizo.
Ielewe nafasi yako na uhakikishe unaisimamia nafasi hiyo kwa gharama zote. Hiyo ndiyo maana halisi ya wewe kuendelea kuwepo katika Dunia hii. Kama ni muimbaji imba kweli kiasi ambacho hata vizazi vitakavyokuja, vikiri kama alikuwepo muimbaji katika Dunia hii. Kama ni mwandishi andika haswa, mpaka vizazi vitakavyokuja miaka elfu baada yako viuone uhai ndani ya maandiko yako. Kama ni mjasiriamali fanya ujasiriamali kwa namna ambayo, uwepo wako utaendelea kuwa na umhimu mkubwa sana katika Dunia hii hata baada ya wewe kuondoka. Kama ni mwalimu fundisha kweli kiasi ambacho mafundisho yako yataendelea kudumu vizazi hadi vizazi. Kwa nafasi yoyote uliyonayo, hakikisha unaisimamia kikamilifu na kuwa tayari kujitoa kama sadaka kwa ajili ya nafasi hiyo.
Kama hauifahamu nafasi yako katika Dunia hii basi itafute. Kumbuka "Hatari kubwa zaidi siyo kifo ila yale bora tunayoyaruhusu yafe ndani yetu wakati huu ambao bado tuko hai" Mzee wetu J.P. Magufuli amelala kishujaa, tuzifuate nyayo zake kwa kujitoa kikamilifu kwa ajili ya kuzitafuta na kuzisimamia nafasi zetu kweli kweli!
RIP JPM tutakuenzi kwa vitendo, umetufundisha kujituma tutajituma baba, hakika uliishika mioyo yetu ikajawa na tumaini la kujituma kufanya kazi, umetufundisha kuwa jasiri tutakuwa jasiri kila tupitapo. Umetufundisha kutafuta maisha ya halali tutafanya hivyo.
Ni mimi "ellyskywilly"