Shuhuli za kijeshi zinazofanywa na URUSI zaitisha Poland na USA

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Marekani kuongeza wanajeshi wake Poland

Rais Donald Trump wa Marekani amesema anafikiria kuongeza idadi ya wanajeshi wa nchi hiyo walioko Poland baada ya rais wa Poland Andrzej ( AND ZEI) Duda, kupendekeza kuwepo kambi ya kudumu ya wanajeshi wa Marekani nchini humo itakayopewa jina la Trump. Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani White House kilichohudhuriwa pia na Duda, Trump amesema Poland mshirika wa NATO iko tayari kuchangia zaidi ya dola bilioni mbili kwa ajili ya kambi hiyo. Trump amesema kuna umuhimu wa Marekani kufikiria ombi la Poland hasa kwa kuwa baadhi ya nchi tajiri washirika wa NATO hazitoi mchango wa kutosha kuhusiana na masuala ya ulinzi kama Marekani inavyofanya. Wasi wasi unaohusiana na kuongezeka kwa shughuli za kivita zinazofanywa na Urusi umeisababisha Poland kuongeza idadi ya sasa wanajeshi wa Marekani 3,000 walioko nchini humo kwa mfumo wa kupokezana na kutaka uwepo wao uwe wa kudumu
images(11).jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom