Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 38,844
- 90,300
SITAKI KUKUMBUKA
Na. Robert Heriel.
Mwanzoni kabisa nilikuwa naamini kuwa Mimi ni moja ya watu wenye ujasiri. Kijana nisiye na woga popote nilipo. Hivyo ndivyo nilikuwa naamini lakini kumbe bhana nilikuwa najiongopea. Kumbe mimi ni jasiri kwa mambo mengi lakini sio mambo yote. Kumbe mimi sio mwoga kwa mambo mengi lakini sio yote. Hilo jana nililitambua.
Nilihisi nipo katika ndoto mbaya sana ambayo nilitamani ikate lakini haikuwa ndoto bali ilikuwa ni tukio halisi. Awali niliwahi Kuona matukio kama haya kwenye Luninga hasa filamu za Kizungu lakini jana nililiona kwa macho yangu ya nyama.
Kwa mara ya kwanza niligundua kuwa hata mimi ni muoga. Niligundua kuwa hata mimi sio jasiri. Nilijihisi kama Panya mwenye wasi wasi mwingi. Jamani itoshe kusema niliogopa haswa.
Ajali ya moto ya jana nilikuwa miongoni mwa mashuhuda. Nilijihisi nipo kwenye filamu ya kutisha sana. Hakika siku ya kifo msaada hukimbia. Hicho ndicho nilikiona siku ya jana.
Ikiwa ni mida ya saa mbili mbili kama sio saa moja nikiwa maeneo ya Msamvu Stendi nilisikia Mshindo mkubwa ukifuatiwa na Moshi mweusi uliofunika Anga lote na kulifanya kuwa jeusi kama wingu la masika. Moto mkubwa ambao sikuwahi kuuona tokea nizaliwe ulifoka na kutamba katika anga.
Kelele na watu kukimbia kimbia vilichukua nafasi. Sikuamini nilichokiona umbali wa mita mia moja nikitokea upande wa Shule ya msingi mafisa karibu na kiwanda cha uchapaji.
Lilikuwa tukio baya lililofanya siku yangu iwe ngumu sana. Nilikiri pale pale moto ndio adhabu mbaya kuliko adhabu yoyote. Kifo cha moto ni kigumu jamani. Ni kifo cha kikatili na maumivu makali sana.
Watu walioungua ngozi mwili mzima wakiwa kama walivyozaliwa walikuwa wakikimbia kuja kule tulipokuwa sisi. Walilia sana nakosa lugha ya kuelezea namna walivyokuwa wakilia. Kila mmoja aliyekuwa shuhuda pale alibaki ameduwaa asijue afanye nini.
Wanawake walilia kama watoto wadogo. Wakiwalilia wahanga wa moto. Sisi vijana na wazee tuliokuwa pale tulihangaika bila kujua tunahangaika nini.
Milipuko kadhaa ilitufanye tukimbie tukikanyagana. Ilikuwa vita. Yaani ukisikia Puuuu! Tunakimbia kama kondoo aliyeona Mbwa. Sitaki kukumbuka tukio la jana.
Sitaki kukumbuka watu niliowaona wakigara gara huku wakiteketea kwa moto mpaka mifupa. Niliona kwa macho sio kwa kuhadithiwa. Ni tukio ambalo kama nitalisahau basi nitakuwa mzee wa miaka mingi sana.
Mdada mmoja aliyekuwa akiungua huku ngozi yote ikiwa imetoka. Alikuwa mweupe pee mwili mzima.
Ndugu zangu ni bora uhadithiwe au uone kwenye luninga kwani utadhani maigizo lakini kuona live unaweza ukafa kwa presha au kuwa mwendawazimu.
Sitaki kukumbuka maneno ya yule dada. Aliongea kwa uchungu akitufuata huku mwili wote umeungua.
''Nisaidieni jamani, nakufa jamani''
Yalikuwa maneno mafupi lakini yaliniingia moja kwa moja. Sikuwa na msaada wowote. Nasikitika sikuweza kumsaidia zaidi ya watu wote tukamkimbia. Alidondoka na kuaga mashindano pale pale.
Nisamehe Sana Dada nilishindwa kukusaidia. Sitaki kukumbuka ulivyokuwa ukiniangalia hali iliyonifanya niwe na woga kupitiliza. Nisamehe Dadaangu.
Dakika kama kumi na tano kwenda ishirini Polisi walifika upande niliokuwepo. Kwa kweli muda ule bado moto ulikuwa mkali. Na kama huna elimu ya moto wa petrol unaweza kujikuta na wewe ni sehemu ya wahanga.
Polisi walijitahidi kuzuia watu wasisogee karibu na ule moto. Kwani bado milipuko midogo ilikuwepo. Watu ni wabishi sana.
Mtu amebahatika kunusurika. Alikuwa ni miongoni na wachota mafuta lakini wakati amepeleka mafuta huko anapojua. Amerudi nguo zote zimelowa mafuta lakini naye anajisogeza karibu na moto. Sitaki kukumbuka kilichotokea. Moto wa petrol jamani jamani. Moto unakuja kama mshale. Ghafla aliliwaka ndani ya sekunde kadhaa hakuwa yeye alikuwa mweupe pee.
Sitaki kukumbuka kijana mmoja akiruka ukuta kutoka kiwanda cha Uchapishaji. Japo alinusurika lakini aliungua. Alilia kama mtoto mdogo.
Sitaki kukumbuka nilisikia wapo wapita njia waliokumbwa na janga hilo. Hawa walishangaa tuu moto unawala ingawa walikuwa hawahusiki na uchotaji mafuta looh!! Mungu awarehemu.
Katika kuuliza nikagundua kuwa chanzo cha ajali ni wezi wa mafuta. Masikini tamaa mbele mauti nyuma ndivyo tunavyoweza kusema. Ni tukio la uhalifu ambalo ni kosa kisheria. Lakini maisha ni maisha tuu. Mungu awasamehe ni shida za dunia tuu.
Wengi wao walikuwa vijana wa bodaboda. Hawa walikuwa na kazi kabisa. Kwa siku boda boda asiyemzoefu hupata kwa siku sio pungufu ya elfu kumi. Kwa wazoefu hulaza mpaka elfu arobaini.
Mama ntilie nao kwa siku kima chini hulaza elfu kumi. lakini kumbe hazikuwatosha masikini Looh!!
Waliacha kazi zao halali. Waliacha kazi zao zenye heshima kwa Mungu. Tamaa ikawaponza. Mungu wangu wasamehe.
Waliojitahidi kubeba mafuta mengi yaani mtu mmoja mmoja sio zaidi ya lita hamsini. Lita moja ya Petrol haizidi elfu tatu. Ni kusema 50×3000=150000. Laki na nusu. Hao ni kwa waliojitahidi sana japo huenda wapo waliozidi hapo.
Tukio la jana linaumiza sana. Ukilifikiria kwa pande zote. Linatupa uchungu, linatupa mafunzo, Lakini pia limetupa athari hasi kutokana na ongezeko la Wajane, Yatima na Wagane. Pia limeongeza kundi la watu wenye ulemavu. loooh!! Inasikitisha sana.
Mbali na hatari ya Petrol lakini Tukio la jana linatukumbusha sisi tuliobaki mambo yafuatayo;-
1. TUACHE TAMAA
Biblia inasema Usitamani mali ya jirani yako. Hiyo ni amri ya msingi wa maisha. Kama watu wasingekuwa na tamaa ya Mali isiyowahusu tukio la jana lisingekuwepo kabisa. Mwalimu wangu wa udereva aliwahi kusema kuwa hakuna ajali ya bahati mbaya. Tulimbishia lakini yeye alibaki na msimamo wake. Yeye ni afisa usalama barabarani.
Tamaa mbele mauti nyuma. Dunia imefikia hapa kwa tamaa. Wapo wenye tamaa za ngono, Tamaa ya madaraka, tamaa ya utajiri na watu hawa ndio huiharibu nchi na dunia kwa ujumla.
2. Wizi sio Mzuri.
Tukio la jana ni tukio la wizi. Tamaa hupelekea mtu kufanya wizi. Yale mafuta yanamwenyewe. Watu walivamia na kuyaiba bila idhini ya mwenye nayo. Lile ni kosa kisheria. Kama moto usingetokea mmiliki wa mafuta yale alikuwa na uwezo wa kufanya msako wa wezi wa mafuta.
Usiseme yalikuwa yanamwagika. Hata kama yanamwagika sio yako yaache yamwagike tuu. Ona sasa.
Amri ya Mungu inasema Usiibe. Mungu tukumbushe kukutii.
3. Usiache kazi yako kisha uvamie yasiyokuhusu. Fata yako.
Walioenda pale karibu walikuwa na kazi zao. Wapo mama ntilie, Bodaboda, Machinga n.k. Waliacha kazi zao. Mungu tusaidie.
Wapo walikuwa wakishangaa shangaa tuu wenzao wakichota mafuta. Hawa ni wapita njia.
Japo hatuwalaumu lakini ni fundisho kwa waliobaki.
4. Umuhimu wa Elimu.
Hapa ni elimu ya vitu hatari kama kemikali, Petrol, Diesel na mafuta ya taa. Milipuko.
Lakini elimu kubwa hapa ni elimu ya dini ya kushika amri za Mungu. Sio kwa vile watu wanaelimu ndio waibe vitu visivyo vyao.
Nimalize kwa kusema tukio la jana ni tukio letu sote kama taifa. Limejeruhi hata wasiohusika ambao sio wachota mafuta.
Mungu azilaze roho za Marehemu mahali zinapostahili. Pia majeruhi tunawaombea wapone. Wasikate tamaa na hali iliyowakuta. Mungu ndiye muamuzi wa mwisho na ndiye faraja kwetu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300