Shettedenis
Member
- Aug 18, 2013
- 49
- 9
Kumekua na wimbi kubwa la raia wa ki china kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ndani ya nchi yetu tukufu. Malalamiko mengi yamejitokeza kuhusiana na uhalali wa shughuli za wachina hawa, hasa karakana na viwanda bububu mitaani. Baadhi ya watanzania kutokana na ugumu wa ajira wamekua wakifanya kazi kwa wachina hawa. Ushauri wangu, serikali ifanye zoezi la kurasimisha shughuli zote zinazofanywa na wachina. Urasimishaji uzingatie sheria za nchi.