Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Takribani wasimamizi 272 wa uchaguzi nchini Indonesia wamefariki dunia baada ya kuugua maradhi yaliyosababishwa na kufanya kazi zinazohusiana na uchaguzi kwa muda mrefu bila ya kupumzika.
Msemaji wa tume ya uchaguzi ya Indonesia , KPU, Arief Priyo Susanto amesema idadi hiyo ni ya hadi jana usiku, huku wengine 1,878 wakiwa wanaugua maradhi hayo.
Susanto amesema wizara ya fedha hivi sasa inashughulikia kuwalipa fidia familia za wahanga wa maradhi yaliyochangiwa na uchovu na wizara ya fedha ikiahidi kuwapa siku za mapumziko watumishi hao.
Uchaguzi wa Indonesia uliofanyika Aprili 17 ulihusisha kura ya rais, bunge pamoja na chaguzi za serikali za mitaa, ambapo wapiga kura takriban milioni 193 walishiki zoezi hilo. Uchaguzi huo unaotajwa kuwa mgumu kabisa duniani, ulihusisha wasimamizi takriban 6,000,000 katika vituo 810,000.