Shubuda asuta wanafiki wanaomfikishia majungu

Mkulima

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
1,033
1,020
Wabunge mnaoongoza kulia lia kila siku, igeni mfano wa Shibuda.

Shubuda asuta wanafiki wanaomfikishia majungu

Friday, 18 September 2009 16:06 Na Suleiman Abeid, Maswa

MBUNGE wa Jimbo la Maswa mkoani Shinyanga Bw. John Shibuda amewakemea watu wanaomfuata kwa lengo la kumtahadharisha kuwa jimbo lake limevamiwa na watu wanaotaka kugombea ubunge na kusema kuwa hataki kusikia maneno hayo kwa vile mtu yeyote ana haki ya kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Bw. Shibuda alitoa kauli hiyo juzi katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa ambapo aliwataka watu wanaomfuata kumweleza habari hizo kuacha mara moja na kwamba binafsi hatotoa fedha zozote zile kwa lengo la kusafisha hali ya hewa jimboni.

"Mimi simzuii mtu kuwa Mbunge wa Maswa kwa sababu kuwa na mtoto wa kike huzuii mtu kuleta posa, niliishatangaza na ninaomba mtu asijisumbue kuniambia Shibuda kuna watu watano wamekuja wanataka kugombea!!, ni haki yao, ohh ninaomba hela, sina hela, siwapi!!", aliweka wazi Bw. Shibuda na kuongeza"


"Tuwashughulikie wanaopitapita kupika majungu, acha wapige majungu sina hela ya kuwapa kwa ajili Shibuda niwe mbunge, sina pesa za kununua kadi za CCM kwa ajili niongeze wanachama wa CCM kunipigia kura za maoni sina!! Nasema sina wala sitatoa hata senti tano," alieleza Bw. Shibuda.

Bw. Shibuda aliwatahadharisha wanaCCM kuwa makini na kadi bandia za CCM ambazo zimeanza kuchapishwa na kusambazwa zikifanana na zile halisi za chama hicho na kwamba tayari makao makuu ya Chama wanashughulikia tatizo hilo.

Alisema binafsi yake hatamnunulia mtu yeyote kadi ya CCM ili aje ampigie kura wakati wa kipindi cha kura za maoni na kwamba ni bora wamnyime kura.

Alikemea tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia jina la Rais Jakaya Kikwete kuwatisha wananchi kutokana na kudai kuwa wapo karibu na Rais na kwamba watu hao waepukwe ni waongo.

"Wale wote wanaojitangaza kutumia jina la Rais Kikwete nawaomba wakome, kwamba wao wameagizwa na Rais Kikwete, wameagizwa na Mzee Makamba, ni waongo, hakuna anayemfahamu Rais Kikwete kunizidi mimi," alieleza Bw. Shibuda na kuongeza;

"Lakini msiwatishe wananchi na watendaji kwa kutumia dhamana zenu za kisiasa ama za mamlaka ya kisiasa yoyote, watumishi chapeni kazi, tupo hapa kutumikia itikadi na dini zote, katiba ndiyo baba na mama na kanuni na sheria za nchi," alieleza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom